Logo
Slay Queen SP Billboard
channel logo dark

Slay Queen

160Drama16

Chris anataka uhuru wake - Slay Queen

Habari
30 Novemba 2020
Kosa kubwa la Chris ni kumpenda Nana kuzidi anavyo jipenda mwenyewe, sasa hivihilo kosa limemgharimu kila kitu.
20201130 115712

Chris amelipaga sana na Nana tangu mara ya kwanza ya kumuona. Nana ni mzuri na mpole, kitu ambacho kilimvutia Chris sana. Mapenzi yao yalikutana na changamoto, na changamoto yao kubwa ilikuwa mama yake na Nana. Mama yake Nana alikuwa anataka Nana awe na mwanaume tajiri. Hakujali kama huyu mwanaume yuko kivipi na ni jinsi gani tabia yake iko akiwa na Nana. Kwa jinsi Nana alivyompenda Chris alikataa kuanza mapenzi na mtu mwingine.

Mama Nana alijifunza kwamba Daktari Kileo alikuwa anampenda Nana na akamsukumizia mwanae aanze mapenzi na Dk. Kileo ingawa Dk. Kileo aliwa anaweza kuwa baba yake na Nana na ana mke na watoto wazima nyumbani.

Dk. Kileo alimuachisha kazi Nana na kumpangia nyumba nzuri, mama yake alifurahi sana. Lakini moyoni Nana alikuwa bado anamuwaza Chris. Nana akaanza kukutana na Chris kwenye nyumba Dk. Kileo aliyo mpangia na alivyo gundua aliamuwa kumteka Chris.

Alimlewesha dawa na kumuweka ndani kama kichaa. Familia ya Chris ikaamini ni kichaa na hamna jinsi ya yeye kutoroka. Je unafikiri Dk. Kileo atazidi kumteka Chris mpaka lini?

Usikose kuangalia #SlayQueenTZ kila Jumatano mpaka Ijumaa saa 3:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160.