Kipindi cha Shilawadu Xtra ni moja wapo ya kipindi pambe chenye heka heka za aina yake, burudani ndani yake ni mambo yanayo endelea katika jamii zetu na mitandaoni kila siku, vijana hawa wawili maarufu kama Soudy Brown na Kwisa kila wiki wanafanya juu chini kupanda milima na mabonde kuhakikisha hatupitwi na tunapata ubuyu exclusive kabisa. Kama ilovyo adaa Shirika la Wambea Duniani ni kipindi cha kusema ukweli na umbea wa mastaa na nyepesi nyepesi za mitaani huku kwetu Tanzania.
