Logo
sarafu
channel logo dark

Sarafu

160DramaPG13

Yaliojiri katika Sarafu wiki hii

Habari
26 Februari 2020
Wakati Madam Sandra kaanza kujipanga upya mipango ya Njoroge pia inaenda sawa.
sarafu, maisha magic bongo

Tanya na Njoroge wanakutana hotelini ili kupanga vile watakavyo wekea Jumba mtego na kumnasa. Damian anaenda kuomba msaada kwa Chaku amsaidie kujenga barabara za juu yaani flyovers. 

Tito nae analeweshwa na anaishia kulala na Brenda. Je, Janet akigundua itakuwaje? Damian anaendelea kusuka mipango yake ya kuifufua kampuni nae Tito kamkia nyumbani kwa Brenda.

Zawadi mambo yashakuwa mabaya na madam Sandra na Jumba nae kawekewa mtego na umemnasa. Madam Sandra anaomba Janeth waungane ili waweze kupambana na Mzee Sanga pamoja. Lakini Janeth pamoja na babake wanagundua kwamba Madam Sandra amebalisha jina ya kampuni na kuweka jina lake. 

Benki inakataa kumpa Damien mkopo. Wanamshauri awekeze nyumba yake kwa benki ili aipate. Damien anaamua kupatana na shangazi ili apate mawaidha. Majadiliano yao inafanya Damian kugundua siri kuhusu babake. Je itamsaidia au mambo yataharibika kabisa?

Tazama highlights hapa:

Tito anakutana na Janeth na anakuwa na wakati mgumu kujieleza kule alikotoka haswa kwa vile Janeth aliona 'love bite'. Je, uhusiano wake na Brenda itajulikana?

Fuatilia tamthilia ya Sarafu kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku ndani ya DStv160 usikose!