Logo
sarafu
channel logo dark

Sarafu

160DramaPG13

Brenda apata kichapo — Sarafu

Habari
05 Machi 2020
...baada ya Janet kupata saa ya Tito chumbani mwake.
sarafu

Wiki iliopita, Tito na Brenda walikuwa kitandani pamoja wakati Janet alikuwa na wasiwasi kwa sababu Tito hakulala nyumbani. Alianza kumshuku pale walipokutana hotelini na kumuuliza wazi kule alikokua. Tito akamdanganya na yakaishia hapo.

Siku iliofuata, Janet alimtembelea Brenda na pale akaona saa ya Tito. Wakati alimuuliza Brenda hio saa inafanya nini pale hapo akasema alikua kwake. Alikula kichapo cha maana na baada ya hapo Janet akaishia kwenda kulewa chakari. 

Kampuni ya Mzee Sanga kampuni kabaki kivuli tu. Je atafanya nini akigundua mali na pesa zote zipo mikononi mwa Madam Sandra?

Zawadi anusurika kutekwa na Tito anampigia magoti Janet huku Jamila na Damian penzi lao liko matatani. Madam Sandra mwisho wake unakaribia,  Jumba nae kafanikiwa kutekwa na Bianca na lakini wivu ya njoroge wivu kwa Bianca unapamba moto.

Mzee Sanga kakimbilia mafichoni baada ya kugombana na Madam Sandra. Baada ya Jamila kushuhudia ya Damian, Chaku hambakishi halafu Madam Sandra ameumizwa na kulazwa hospitality.  Je, Janet ataungana na mama yake?  Na je kwa alichokifanya Jackie usalama wake utakuwepo kweli?

Ungana nasi kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku ndani ya Dstv 160 #MMBSARAFU