Logo
Sarafu Slim Wahusika
channel logo dark

Sarafu

160DramaPG13

Panda shuka katika Sarafu

Habari
29 Januari 2018
Wakati mashabiki wanaingoja kwa hamu sehemu ya saba ya tamthilia ya Sarafu, hebu tuangalie yaliojiri wiki tatu zilizopita!
Screen Shot 2018-01-29 at 16.27.18

Wakati mashabiki wanaingoja kwa hamu sehemu ya saba ya tamthilia ya Sarafu, hebu tangalie yaliojiri wiki tatu zailizopita ! Chuki kati ya Eng. Sanga na Eng. Samwel inazidi kupamba moto  huku kila mmoja akifanya juu chini kumteketeza mwenzake, na vita vyao sasa vimekua vya nyama kwa nyama.

Huku wake zao nao wakiwatuhumu  kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengine.

Jacky na Janeth Sanga ni mabinti wa Eng. Sanga. Kila mmoja ana matatizo na changamoto zilizotoka katika familia. Jacky anahisi wazazi wake hawampendi kama wanavyompenda Janeth na Jacky anaishi Maisha yake kuwakomoa, na kuwa na mahusiano na adui mkubwa wa baba yake.

Kwa maslahii zaidi Isitoshe Chuma ni mpenzi wa Jacky ambaye  yuko gerezani. Anajaribu juu chini kushikila penzi lao, lakini huku uraiani Jacky anapambana kiume na anaishi Maisha ambayo Chuma hajui chochote, je mahusiano yao yataishia wapi?

Usaliti nao haukuachwa nyuma. Eng. Sanga yuko hatarini kwa kuwa kila mmoja yupo kizania kwa upande mwingine Damian na baba yake Eng. Samwel wanaingia katika uhasama wa mapenzi  baada ya baba yake kutembea na mpenzi wake Janeth, aliyetumwa na baba yake kumlaghai Na mwenyewe akiwa na nia zake binafsi! 

Pata kipindi cha kwanza hapa, kisha, jitayarishe kuendelea na kipindi cha saba Jumatano, saa 1.30 usiku hapa Maisha Magic Bongo!