Logo
Small billboard rebeca
channel logo dark

Rebecca

160DramaPG13

Burudani halisi mwezi huu wa Aprili!

Habari
06 Aprili 2018
Tumefika mwezi wa Aprili na hapa #MMBongo ni kazi tu! Pata kujua tuliyowaandalia katika habari hii!
<p>Screen Shot 2018-04-05 at 15.24.49</p>

 

Mwezi huu tunawaletea filamu za kila wiki! Simulizi ya Nusaiba ni ya kusikitisha. Mke wa Bamkuza aliyependwa sana na mume wake, anayo shida ya kutopata mtoto. Familia ya Bamkuza wanamdharau sana Nusaiba. Changamoto zake zitafikia wapi? Tazama filamu ya leo, Nusaiba saa 2 usiku hapa #MMBongo

 

Tamthilia mpya ya #MMBRebecca imeshika moto! Hadithi ya Rebecca inaendelea kusisimua! Usikose vipindi kila wiki kila Jumatatu hadi Jumatano saa 3 usiku kupitia DStv chaneli 160!

 

Muziki wetu wa Bongo Fleva moto moto na video mpya kutoka wasanii mashuhuri hapa Tanzania kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 jioni! Pata habari zaidi kutoka ulimwengu wa burudani katika kurasa zetu za kijamii na video zetu katika chaneli ya Maisha Magic Bongo YouTube.

 

Tamthilia ya Sarafu na Kapuni kwa pamoja zimechuna vilivyo na wahenga walisea kila chenye mwanzo kina mwisho, hivyo basi tamthilia hizi mbili kwa sasa zitaendaa kwenye mapumziko kidogo. Na zitarudi hewani hivi karibuni.

 

Tukingojea msimu mpya wa #HUBATZ hivi karibuni , pata marudio yake  kila Jumatatu hadi Ijumaa, saa 11 jioni hapa #MMBongo!

 

Bi Mariam wa Migomba anarudi katika runinga yako mwezi huu na mada zake moto moto tunakuhakikishia tutacheka, tutalia lakini kubwa Zaidi tutajifunza mengi sana kuhusu Maisha ya kila siku, jinsi ya kuishi na wanajamii wenzetu na kadhalika masomo haya yatasindikizwa na burudani ya taarab kila Jumatano saa 1 usiku katika kipindi mkipendacho, Mchikicho wa Pwani. USIKOSE!