Logo
Small billboard rebeca
channel logo dark

Rebeca

160Drama6

Mambo yamewaka MOTO! — Rebeca

Habari
28 Februari 2019
Rebeca wiki hii imekua na msisimko machozi kasheshe na jazba kila kona!
Mambo yamewaka MOTO!  — Rebeca

Hatimaye Rebeca ameruhusiwa kutoka hosipitali, bibi yake akimshika mkono katika wakati huu mgumu, nyumbani anakutana na vita vya aina yake

Baba yake kapoteza kampuni, badala kupambana kupata kampuni yake ndio kwanza anaponda raha Michele.

Wazazi wa Cleopatra wamegundua ukweli kuhusu Kambona na binti yao na haya yote yakiendelea Deo anarudi amefanya maamuzi kuhusu  mtoto wake, Cleo na mama yake waanachwa roho juu, wiki ijayo tutajua kama alimchukua mtoto au laa.

Monji ni mjamzito, akiwa anampa Daniel hizo taarifa Daniel anamjulisha ya kwamba yeye na Rabeca bado ni mke na mume , Monji jazba juu fatilia kitakachoendelea kati yao wiki ijayo.

Gallery

Usikose kupata uhondo cha Rebeca kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku ndani ya DStv 160 pekee!