Logo
Pazia
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia16

Tuanza Aprili na misimu mipya ya tamthilia uzipendazo

News
04 Aprili 2023
#MMBPazia, #MMBHuba,#MMBJuaKali na #MMBMwali zaingia kwenye misimu mipya!
Pazia

Tunafurahia kuwatangazia kwamba baadhi ya vipindi vyenu pendwa vya Maisha Magic Bongo vinarejea tena na misimu mipya ndani ya mwezi wa Aprili. Hii ni nafasi ya kufurahia hadithi zenye kusisimua na zenye kujenga, zinazokwenda sambamba na tamaduni na maisha ya Watanzania.

Kwa wapenzi wa #MMBPazia, sasa tunaingia ndani ya msimu wa sita. Fuatilia changamoto za mapenzi kati ya Bidu na mke wake na pia, Regina na Edu wakiwa wanapambania ndoa yao. Kumbuka kuangalia vipindi vipya kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku.

Wapenzi wa #MMBHuba Tamthilia yetu knongwe kabisa bado inarindima vilivyo katika msimu wa kumi na mbili. #MMBHuba imekuwa moja ya vipindi vinavyosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Televisheni nchini Tanzania. Hapa, tutapata kujifunza kuhusu maisha ya mapenzi ,  usaliti, tamaa na majivuno  jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kuibuka. Hivyo, ni msimu wa kuvutia n awa kusisimua kabisa kwa kifupi tunakuja kivingine kabisaa kaa mkao wa kula #MMBHuba, jiunge  nasi kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku.

Kwa wapenzi wa vichekesho na kuvunja mbavu, msimu mpya wa #MMBKitimtim umeanza na umeshaleta msisimko kwa watazamaji wake. Katika msimu huu, tutashuhudia jinsi ndoa za mabadiliko katika familia ya  Pili, anaolewa na mtu mwingine kisa madeni ya mumewe panda shuka na maisha yao hakika yatakuacha hoi msimu huu . Usikose kuangalia #MMBKitimtim kila Jumatatu na Jumanne saa 3:30 usiku

#MMBJuaKali inaingia katika msimu wake wa sita. Vipindi hivi huonyesha jinsi ya kuwa na nguvu na ujasiri katika maisha na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kifamilia , Professa anaonyesha kutojali kabisa maisha sio ya Watoto wake tu bali kila aliyemzunguka , Je hatma ya kila mtu ni nini haswa na je Professa afanywe nini aache kuvuruga watu , uhondo kupitiliza katika tamthilia hii ya Taifa kila Jumatano-Jumapili saa 3:30 Usiku

Kwa upande wa #MMBMwali, tamthilia hii itakuwa inaingia katika msimu wa pili. Fuatilia mahusiano ya Nozo na Mwali kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku kujua kama penzi lao litadumu.

Usikose kufuatilia misimu mipya ya #MMBPazia, #MMBHuba, #MMBKitimtim, #MMBJuaKali na #MMBMwali, kila siku kuanzia mwezi huu wa Aprili kupitia chaneli 160 ya DSTV.

MISIMU MIPYA YA VIPINDI VYA MAISHA MAGIC BONGO!

Ni msimu mpya wa kipindi gani unakipenda zaidi?

Pazia13%
Huba16%
Kitimtim26%
Jua Kali40%
Mwali5%