Logo
Mengine Zaidi
channel logo dark

Pazia

160TamthiliaPG13

Waridi na Jemo – Pazia

Habari
10 Juni 2022
Baada ya kuchwa Edu, Waridi afanya mpango mwingine wa kurudiana nae.
Untitled design (1)

Baada ya mambo kutoenda sawa kwenye ndoa ya Edu na Regina, Edu alijikuta mikononi kwa Waridi. Waridi alikuwa akimtumia Edu ili aweze kuridhi mali ya bibi yake. Kabla ya kifo cha bibi yake na Waridi, aliweka maandiko kwamba Waridi arithi mali yake baada ya kuolewa. Tatizo lilikuja baada ya Edu kuanza kufanya uchunguzi wa kujua wazazi wake halisi walikuwa nani, kwa sababu yeye alikulia kama mtoto yatima. Wakati Edu na Waridi walivyokuwa wakifanya uchunguzi kuhusu wazazi wa Edu, waligundua kwamba walikuwa ndugu ambao walikuwa na baba mmoja. Baada ya hapo, Edu alikataa kumoa Waridi na alicha mahusiano nae.

Sasa hivi, Waridi amerudi mjini na bado anahisia na Edu. Edu nae ameshaendelea na maisha yake bila Waridi, kwa sasa hivi alipata fedha ya urithi kutoka kwa baba yake na aliamua kuwa mdhamini wa nyumba ya Watoto yatima na hataki mahusiano na Waridi.

Waridi aamua kukutana na Jemo, kwa sababu Jemo anahitaji pesa, ili wajifanye kama wapo kwenye mahusiano ili Edu awaonee wivu na arudi kwa Waridi. Muda huu wote Waridi alikuwa akimlipa Jemo ili Jemo aendelee kuwa nae na sasa hivi anadai mtoto. Je huu mpango utaweza kumrudisha Edu kwa Waridi?

Untitled design (1)
Waridi na Jemo - Pazia

Je unafikiri mahusiano ya Waridi na Jemo yatamfanya Edu arudi kwa Waridi? Tuambie

Ndiyo42%
Hapana58%

Kwa sasa hivi Edu ameamua kusonga mbele na maisha yake, itawezekana kwamba baada ya kurudiana na Waridi ataweza kurudi nyumba tena. Usikose kuangalia #MMBPazia kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo!