Logo
Mengine Zaidi
channel logo dark

Pazia

160TamthiliaPG13

Msimu mpya wa Pazia waanza na moto mkali!

Habari
07 Aprili 2022
Pazia irejea ndani ya #MaishaMagicBongo kwa ushindi
MMB PAZIA S4 FB COVER GENERIC

Msimu mpya wa #MMBPazia warejea kwa nguvu ya ajabu. Tuaanza msimu baada ya miaka mitano kupita na Maisha ya watu wote ndani ya kipindi hiki yame badirka sana.

Regina

Msimu wa mwisho wa #MMBPazia uliishia na Regina akijifungua mtoto wa kike. Sasa hivi huyu mtoto ameshakuwa na kashaanza shule. Sasa hivi Regina na mwanae wanaishi na mama yake Miriam na Regina ndio ameanza kazi mpya ndani ya kampuni ya Bwana Mdoe.

Miriam

Msimu uliyopita uliishia na Miriam kurudi nchini baada ya kutoroka na Mdoe. Kwa sasa hivi Miriam anaishi kwake na Regina pamoja na mwanae. Matatizo ya mkumba Miriam baada ya kugundua kwamba anadahiwa pesa nyingi nah ana kazi.

Gloria

Msimu wa mwisho wa #MMBPazia, Eliza aligundua kwamba mwanae, Gloria, bado alikuwa anaendelea kutembea na Henry. Kwasababu hiyo, Eliza alimpiga bastola Gloria na kwa bahati nzuri gloria hakufariki. Ila kuokoa maisha yake, aliamua kukimbia kijijini.

Eliza

Baada ya kuona kwamba Henry bado alikuwa akitembea na Gloria, na baada ya kumpiga bastola Gloria, Eliza aliamua kurudiana na Mdoe. Kwa sasa hivi, Eliza bado anamtafuta Gloria na anataka kumuua.

Mdoe

Baada ya kuachana na Miriam, Mdoe aamia na Eliza. Kwa sasa hivi, Mdoe amemuajiri Regina n ani kwasasababu bado anadhani kwamba Regina bado ni mtoto wake.

Angalia watazamaji wetu wanasemaje kuhusu msimu mpya wa Pazia:

Usikose kufuatilia matukio ya #MMBPazia ya msimu huu mpya kuanzia kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 ndani ya DSTV chaneneli 160!