Logo
Mengine Zaidi
channel logo dark

Pazia

160TamthiliaPG13

Henry apaka kazi mpya – Pazia

News
24 Machi 2023
Baada ya kufukuzwa kazi, bosi wake Henry alimrudia na ofa mpya ya kazi
Article

Henry amekuwa akipitia magumu na baada ya kutoka jela, alijikuta amepoteza kazi yake na hana jinsi ya kutafuta pesa. Baada ya kufukuzwa kazi na bosi wake, alirudi kumuomba nafasi ya kufanya kazi tena na bosi wake aja na mpango mpya wa kumtafutia kazi.

Mama Nana, bosi wake na Henry amekuwa akisumbuliwa na mtoto wake Nana juu ya tabia yake, na anaamini kwamba mtoto wake anahitaji mwanaume anaye mheshimu katika maisha yake.  Kwa hiyo, mama Nana amemwambia Henry aseme kuwa yeye ndiye baba yake mzazi na kwamba ndiyo amerudi kutoka Kongo.

Henry aliishia kukubali kazi hii lakini anahisi vibaya kuwadanganya watu, hasa Nana ambaye ameanza kumpenda kama baba yake. Lakini anashindwa kufanya chochote kwa sababu ya shinikizo la bosi wake.

Je itakuaje Nana akigundua kwamba Henry sio baba yake na mama yake alimdanganya? 👇

Endelea kuburudika na kipindi cha #MMBPazia kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku!
 
 

Henry apaka kazi mpya – Pazia

Je itakuaje Nana akigundua kwamba Henry sio baba yake na mama yake alimdanganya?

Atakimbia nyumbani75%
Atazidi kuwamtundu zaidi na kumkasirikia mama yake0%
Bado ni mdogo hatafanya lolote25%