Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Watazamaji wa Maisha Magic Bongo wapokea #PaziaTZ kwa furaha

Habari
13 Januari 2021
Mwaka mpya ulianza na mambo mampya ndani ya Maisha Magic Bongo na kipindi kipya cha #PaziaTZ
Screenshot 2021 01 14 at 15

 Kama bado haujasikia sijui wewe ulikuwa wapi? Tarehe 4 Januari 2021, kipindi kipya kiliingia ndani ya chaneli 160. Kipindi hiki kinaitwa #PaziaTZ na kilianza kwa kasi sana, moja kwa moja kulikunata na binti mzuri anayeitwa Regina na ghafra baada ya kwenda kula bata na marafiki zake alipotea na wazazi wake wabaki hoi kumtafuta.

Washabiki wa Maisha Magic Bongo walikuwa wakisubiri kwa hamu sana kipindi hiki baada ya kuanza kuhesabu siku zilizo baki mpaka kipindi kuanza. Ukiangalia jinsi walivyo jibu kwenye mitandao yetu ya jamii inaonekana kwamba kipindi hiki kiliwafurahisha sana. Soma chini kujua maoni ya washabiki wa Maisha Magic Bongo baada ya kuangalia kipindi cha kwanza cha #PaziaTZ:

  1. “Kipindi kizuri sana can u imagine am a banker lakini niliwahi kipindi na kizuri balaaaa…can’t wait for the next episode!” - @emmygracious
  2. “Regina anakaza sana” - @rocky_kunj
  3. “Iko poa sana. DSTV vipindi vyenu quality yan sikutegemea pazia itakua FIRE can’t wait the next ep” - @chichi_magige
  4. “Director Aziz hana kazi mbovu hata kidogo. Big UP!” -@felly255
  5. “Kipindi cha kwanza tuu mshatuteka wengi” - @verodayanamwai
  6. “I love it.The hottest!” - @b.i.n.d.o_g.w.a.i
  7. “Yani iko bomba kweli nimeipenda sana” - @ts_cutevicky
  8. “Muda mfupi jamanii” -@sarfat_cakes
  9. “Ni tamthilia nzuri sana kwa kweli” - @asnathmzinga7
  10. “Ipo vizuri nimeipenda kwa kweli Tanzania tunajitahidi kwenye tasnia ya movie” -@meshack5241

 

Kama wewe ulikuwepo ndani ya asimilia ya watu amabao walikosa kuangalia kipindi cha kwanza cha #PaziaTZ usijali. Pata marudio yake kila Jumapili saa 10 jioni na vipindi vipya kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku ndani ya chaneli 160!