Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Umeshakutana na Brenda na Wadiri? – Pazia

Habari
23 Machi 2021
Wadada wawili wapya wajiunga na #PaziaTZ
Untitled design (8)

Kasheshe hazikosi kuisha ndani ya #PaziaTZ baada ya tamthilia kuongeza waigizaji wengine wapya. Tulikutana na Brenda na Wadiri hii wiki na ndio tunaendelea kuwa fahamu zaidi. Hapa chini ndivyo tunavyojua kuhusu hawa wadada;

Wadiri
Wadiri ni rafiki yake Gloria wa zamani tangu walivyokuwa wadogo. Tunajifunza kwamba, Wadiri aliwahi kuwa mwanafunzi wa Eliza, mama yake Gloria na kwamba Eliza anamkumba kwamba alikuwa na tabia mbaya. Lakini Gloria anamtumia Wadiri kuvunja ndoa ya Edu na Regina kwasababu Edu na Wadiri walishawahai kuwa wapenzi zamani.

 

Brenda
Brenda ni rafiki yake na Fred, wakulia pamoja na wamekuwa kama familia. Fred alikuwa akimsahidia Brenda kulipa ada ya shule lakini sasa hivi hana iyo pesa. Wakati akiwa chuoni, Brenda aanza kusumbuliwa na Ben na Ben amwambia Brenda kwamba anaweza kumsahidia kulipa ada lakini akiwa na mpango wa kumtapeli.

Kumbuka kwamba ukisosa kipindi chochote cha #PaziaTZ unaweza kuangalia kupitia Showmax sasa hivi. Na pia, kumbuka kwamba #PaziaTZ inacheza kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 1:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.