Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Ulichokosa kwenye Insta Live ya Maisha Magic Bongo – Pazia

Habari
25 Februari 2021
Wiki iliyopita Eliza, Jemo na Regina walijiunga na Insta Live kupigastori na watazamaji wa Pazia.
Screenshot 2021 02 25 at 17

Wiki nzima waigizaji wa #PaziaTZ walikuwa ndani ya Insta Live ya Maisha Magic Bongo kupiga story na watazamaji wa #PaziaTZ. Hizi insta live zilivuma sana mpaka tukapata washabiki wa kimataifa waliojiunga na sisi. Kama kuna siku yeyote uliyo ikosa, hapa tumekutolea kiufupi yaliyotokea na kila muigizaji aliyekuwepo.

Eliza

Eliza ni mama yake na Gloria na wana uhusiano mzuri kama mama na mtoto lakini, Gloria ameanza kumkasirisha mama yake kwa jinsi tabia yeke ilivyokuwa mbaya. Eliza anataka kuwa na mahusiano na Henry lakini Henry hamtaki. Watazamaji walikuwa wanataka kujua kama Eliza akuwa na mahusiano na Henry, n ani kituambacho ni lazima uendelee kuangalia Pazia.

Regina

Regina ni mtoto wa Henry na Miriam, sasa hivi ameolewa na Edu na wanaanza maisha yao pamoja. Watazamaji wakuwa wanataka kujua kwanini Regina alichagua kuolewa hospitalini na jinsi mahusiano yake na Gloria yatabadirika baada ya kugundua kwamba Gloria anatembea na baba yake. Pia kwenye Insta Live ya Regina tulijifunza kwamba #PaziaTZ inawashabiki wengi kutoka nje ya Tanzania, tuliongea na watazamaji kutoka Zambia na pia Kenya.

Jemo

Jemo anampenda sana Regina lakini tatizo kubwa ni kwamba Regina hampenda na hivi sasa ameshalolewa na Edu. Tatizo linguine kwa Jemo ni Gloria ambaye anamlazimisha Jemo wawe pamoja.  Swali kubwa watazamaji wa #PaziaTZ walikuwa wanataka kujua toka wa Jemo ni kwamba, anazipata wapi hizo pesa vote wapi.

 

Kama umekosa hizi Insta Live zote tufuatilie kwenye Instagram yetu ya @maishamagicbongo kuangalia hizi Insta Live zote.