Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Ujauzito wa Regina  – Pazia

Habari
12 Mei 2021
Ujauzito wa Regina waleta shida na maisha yake yako mashakani
Screenshot 2021 05 20 at 14

Baada ya kugundua kwamba anaujauzito Regina alifurahi sana lakini furaha yake haiku kaa kwa muda mrefu. Aligundua kwanza kuwa mimba yake ina miezi mitatu wakati yeye na Edu hawakuona kwa muda huo.

Edu alivyogundua umri wa mimba ya Regina hakutaka mahusiano naye. Lakini kwa bahati mbaya mimba ya Regina ilikuwa hatarini kwa sababu mtoto alikuwa anakuwa nje ya mfuko wa uzazi. Hili jambo lilimfanya Regina achague kati ya maisha yake au maisha yam toto wake mtarajiwa.

Regina alichagua kuokoa maisha yam toto wake ili yeye afariki na kwa bahati mbaya alipoteza mtoto.

 

Kwa sasa hivi Regina anajiandaa kurudi nyumbani bila mtoto wake na hajui kama Edu atamkubali. Usikose kuangalia #MMBPazia kila Jumatatu hadi ijumaa saa 1:30 usiku ndani ya chaneli ya Maisha Magic Bongo.