Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Pazi na Harusi Yetu zarejea kwa kishindo! - Maisha Magic Bongo

Habari
25 Machi 2022
Mwezi wa April wakuletea msimu mpya wa Pazia na Harusi Yetu!
Untitled design (17)

Tamthilia iliyozua gumzo mitaani ya #MMBPazia nayo inarejea tena kwa nguvu mpya huku msimu wake wa 4 ukianza Jumatatu Aprili 4, 2022 na itakuwa ikionyeshwa mara tatu kwa wiki kuanzia Jumatatu hadi Jumatano saa moja na nusu jioni. Huku nako kimeumana kwani Regina amejifungua mtoto wao na Edu. Juma Mdoe sasa anaishi na Eliza, Regina alienda kuishi na Mirriam hukua Gloria akiamua kikimbilia kijijini; Huwezi kuamini! Sasa Henry ni mfanyakazi katika duka la vifaa vya ujenzi la Eliza ambalo awali alikuwa analimiliki. Ni nini kimetokea hadi mambo yakabadilika kiasi hiki? Bila shaka hutakubali kupitwa na utamu na msisimko wa tamthilia hii maridhawa ya Pazia.

Kwa wale wapenzi wa kipindi cha #MMBHarusiYetu hawajaachwa nyuma kwani nacho kinarudi kuanzia Aprili 7, 2022 kila siku ya Alhamisi saa 1 jioni. Huku utashuhudia yanayojiri kwenye harusi za watu kuanzia yale yanayojiri nyuma ya pazia. Kwa hakika utaona jinsi harusi zilivyo na mambo mengi nyuma yake!

Ni msimu gani mpya una hamu nacho Zaidi? Tuambie hapo chini👇

Pazia na Harusi Yetu!

Ni msimu gani mpya una hamu nao zaidi? Tuambie hapo chini

Harusi Yetu19%
Pazia49%
Zote mbili32%