Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Ni nani ambaye ni baba wa mtoto wa Regina? - Pazia

Habari
23 Machi 2021
Regina agundua ana ujauzito wa miezi miwili na hajui ni mimba ya nani.
Screenshot 2021 03 23 at 11

Baada ya poteza fahamu na kuamka kwa Fred, Regina hakumbuki kilichomtokea. Regina aliamua kuchua huu muda kumdanganya matukio ya usiko wao, kwasababu Gloria ndiye aliye muwekea madawa ya kulevywa Regina.

Regina alimua kuolewa na Edu na kuanza maisha nae, tatizo ni kwamba Regina amebeba mimba nah ii mimba ni ya miezi miwili wakati ndoa yake na Edu ni ya chini ya mwezi mmoja. Sasa Regina anajaribu ilikuwaje abebe mimba ya miezi miwili na nini kilichomtokea usiku ule alivyo wekewa madawa ya kulevya. Amefanikiwa kuchagua watu wanne ambao wanaweza kuwa baba wa mtoto wake:

 

  1. Edu

Edu ni mume wake na Regina, Regina alimlazimisha Edu amuoe baada ya kuambiwa na Gloria kwamba Edu alimpeleka Regina nyumbani.

 

 

  1. Jemo

Jemo alikuwa anampenda na umtaka Regina kwa muda mrefu lakini Regina hamtaki. Jemo alikutana na Dr. Love kufanya mpango wakumwambia Regina kwamba mimba ya regina ni ya Jemo ili Jemo aweze kuwa na Regina.

 

 

  1. Fred

Fred ndiye aliyekuwa wa mwisho kuonekana na Regina na Regina mwenyewe anakumbuka kwamba alirudi na Fred nyumbani yeyote yaliomtokea Regina, yalitokea nyumbani kwa Fred.

 

 

  1. Dr Love

Watazamaji wote wanajua kwamba Dr. Love ndiye ambaye alimfanyia Regina vibaya. Tatizo kubwa hamna mtu yeyote aliyeshuhudia haya matukio na Regina akumbuki.

 

 

Unafikiri Regina ataweza kugundua hii mimba ni ya nani? Kumbuka kuangalia #PaziaTZ kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 na pia unaweza kuangalia kupitia Showmax.