Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Nani Jemo? – Pazia

Habari
29 Julai 2021
Siri ya Jemo ya gundulika
Screenshot 2021 07 28 at 23

 

Jemo alikuwa anajulikana kama mfanya biashara tajiri kati ya marafiki zake wote. Kila mtu, kuanzia Fred, Regina, Gloria na Edu walikuwa wamezoea kumkimbilia wakiwa na shida nah ii ni kwasababu alikuwa mtu wakutegemewa kukiwa na shida.

Baada ya kukutana na Dkt. Love, Jemo aingia kwenye deni na Dkt Love kwasababu Dkt. Love ndiye aliye msahidia Jemo kumdanganya Regina kwamba mimba ya Regina ni ya Jemo. Walifanya hivi kwasababu Dkt. Love ndiye aliyembaka Regina na alikuwa hataki kwenda jela na Jemo aliona kwamba hiyo ndio njia sahii ya kumpata Regina.

Baada ya Dkt. Love kufukuzwa kazi, aliishiwa pes ana akaamua kumteka Jemo. Tatizo likaja baada ya Jemo kuzidi nguvu Dkt. Love na kuishia kumuteka Dkt. Love. Hapo ndipo Jemo akaapa kumuua Dkt. Love na Dkt. Love alivyo fanikiwa kutoroka alimripoti Jemo polisi.

Walivyofika polisi ndio walivyogundua kwamba Jemo sio mtanzania. Jina lake yeye ni James Ubanga, ni mkimbizi kutoka Rwanda. Alikuja Tanzania kama mwanafunzi, kusoma na aliaamua kuacha masomo na kuwadhurumu wafadhiri wake ili aishi kifahari.

Baada ya haya yote, Maisha ya Jemo yako mashakani nchini Tanzania. Fuatilia tamthilia ya #MMBPazia kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.