Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Matukio ya Finali ya Pazia!

Habari
12 Novemba 2021
Finali ya #MMBPazia ilijaa matukio mengi ya moto mkali.
Screenshot 2021 11 12 at 11

Kipindi cha mwisho cha msimu wa tatu wa #MMBPazia ulionyeshwa ndani ya Maisha Magic Bongo, tarehe 10 Novemba. Kipindi hiki kilijaa matukio mengi ambayo yaliacha watazamaji wa #MMBPazia wawe na hamu nacho na kutaka kirudie  tena. Tangu kipindi cha #MMBPazia kiishe kuna maswali  ambayo watazamaji bado walikuwa wanataka kupata majibu.

Swali la kwanza, ni nani baba yake Regina na ni nani baba yake Gloria? Henry ndiye aliyemlea Regina wakati Gloria alilelewa na mama yake Eliza bila baba. Ingawa Henry na Eliza walishawahi kuwa mume na mke, Gloria alizaliwa baada wao  kuachana. Baada ya kuachana na Eliza, Henry alimuoa Mariam na wakati huo  walizaa Regina. Hatimaye Mariam aliamua kuondoka na kumuacha Henry, wakati huu Eliza alihamia kwa Henry na alimlazimisha Henry kumuoa. Wakati Eliza alivyokuwa kwa Henry alimwambia Henry kwamba Gloria ni mwanae na Regina alikuwa mtoto wa Mdoe. Baada ya kugomba sana na kutaka kujua ukweli, Eliza aliyoboa siri na kumwambia ukweli kwamba alikuwa na mahusiano na Mdoe wakati alivyokuwa ameolewa na Henry na Gloria ni mtoto wa Mdoe wakati Regina alikuwa mtoto wa Henry.

Swali kubwa la pili lilikuwa ni nani baba wa mtoto wa Regina. Edu alipima DNA na iligundulika kwamba yeye ndiye baba wamtoto wa Regina. Kwenye kipindi hiki cha mwisho Regina na Tunu walipata uchungu na wote wawili walizaa watoto wakike. Wakati huu, Sadiq alikuwa na mpango wa kuiba mtoto wa Bidu na Tunu, kwa bahati nzuri muuguzi alimkamata Sadiq na mtoto na kumrudisha lakini akamua kuchanganya watoto. Sasa hivi Bidu na Tunu na Regina na Edu hawajui kama wamebeba mtoto wasio wa kwao.

Kumbuka kwa #MMBPazia iko kwenye mapumziko mpaka mwezi wan ne ndani ya Maisha Magic Bongo!

Pia unawezakupendelea: