Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Maisha Magic Bongo yazidisha uhondo wa burudani

Habari
06 Januari 2021
Tamthilia mpya za Jua Kali na Pazia zaanza kupasua mawimbi ndani ya DStv Bomba
8

Mambo ni bandika - bandua, paukwa – pakawa ndani ya chaneli maarufu ya Maisha Magic Bongo (MMB) ambapo imetangaza rasmi kuanza kwa tamthilia mbili kabambe za Pazia na Jua Kali, zitakazoanza kurushwa kuanzia Januari 2021 kwenye Chaneli ya MMB DStv 160.

 

Kiu ya mashabiki wa tamthilia za kibongo imepata dawa kwani tamthilia mpya ya Pazia imepikwa ikapikika huku ikisimamiwa na mzalishaji maarufu na kijana mtanzania Samwel Isike, ambaye pia ndiye aliyezalisha tamthilia iliyojizolea umaarufu mkubwa hapa nchini ya Sarafu.

 

Tamthilia hii imeaanza kurushwa kuanzia January 4, 2021 na inaonekana Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 Jioni. Tamthilia hii imejaa mikasa, visa, vitimbi bila kusahau mafunzo yatokanayo na maudhui yake. Tamthilia hii imesheheni vinara wa uigizaji hapa nchini akiwemo Jacqueline Wolper anayeigiza kama Miriam Lewa bila kumsahau Hisani Muya anayeigiza kama Henry Lewa

 

Uhondo hauishii hapo, kwani mzigo mwingine unaoshushwa ndani ya MMB ni tamthilia ya Jua Kali kutoka kwa mzalishaji maarufu mwanadada Leah Mwendamseke, ambaye mbali ya kuwa ni mzalishaji wa tamthilia maarufu ya Kapuni pia ni mshindi wa tuzo mbalimbali katika tasnia ya filamu.

 

Tamthilia hii ya Jua Kali itaanza kutingisha jiji mnamo Januari 6, 2021 na itakuwa ikirushwa saa 3.30 usiku Jumatano hadi Ijumaa. Huku nako kuna waigizaji nguli kama  Rainfredd Masako anayeigiza kama Professor Bili na kumejaa vituko na mikasa ya kila aina ambapo wapenzi wa tamthilia hawatapenda kuikosa au kusubiri kusimuliwa.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthilia hizo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo, amesema kuwa serikali inathamini na kutambua mchango mkubwa wa MultiChoice katika kukuza na kuendeleza tasnia ya filamu hapa nchini. Amesema kitendo cha chaneli ya Maisha Magic Bongo kuwa na maudhui mengi ya ndani kimekuwa ni chachu ya ajira nyingi katika tasnia lakini pia kimeongeza ushindani na ubora wa kazi za wazalishaji wetu. Amesema kuwa yeye binafsi amekuwa akiwatemebelea wasanii na kujionea uzalishaji wa filamu mbalimbali hapa nchini na ameridhishwa na kuongezeka kwa ubora na weledi katika uzalishaji wa filamu na maudhui mengine. Amewataka wasanii kutumia fursa hii vizuri na kuhakikisha kuwa wanaongeza ubora wa kazi zao ili ziweze kushindana katika soko la ndani na nje na hivyo tasnia ya filamu kuongeza mchango wake katika uchumi wa wasanii na taifa kwa ujumla

 

Naye Mkuu Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo, amesema mbali na kutumia wasanii na waigizaji wakongwe, wamehakikisha kuwa kuna mchanganyiko na waigizaji wapya na vijana ambao wanaleta vionjo vipya na vya kisasa katika tamthilia hizo na hivyo kuzifanya kuwa kivutio kikubwa kwa watazamaji wa rika zote.

 

“Kila mara tunaleta maudhui kulingana na matakwa ya wateja wetu, tunhakikisha kuwa tunawapatia maudhui yaliyoboreshwa na yenye vionjo vipya kila uchao bila kusahau uhalisia wa kitanzania kwenye maudhui yetu” alisema Ronald na kuongeza kuwa wanafurahi sana kufanya kazi na wazalishaji na waigizaji wa Tanzania na hivyo kuzidi kukuza vipaji vya wasainii wetu na kuwapa ulingo wa kuonyesha umahiri wao katika fani.

 

Amesema kuwa katika miaka 5 tangu chaneli hiyo ianzishwe, mamia ya wazalishaji na wasanii wa Tanzania wamepata fursa ya kuuza kazi zao na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza soko la maudhui hususan filamu hapa nchini.

 

Kuhusu Pazia

Suala la ndoa ni suala takatifu la kuunganisha watu na mioyo miwili inayopendanana na kushibana. Ndoa huleta furaha na umoja kwa wale wanaoitunza. Inakuaje pale ndoa imapochezewa na isipopewa heshima yake? PAZIA inakupitisha katika safari ya mtoto aliyepambana kufa na kupona kunusuru ndoa ya wazazi wake kuvunjika

 

Kuhusu Jua Kali

Katika jamii nyingi, Maisha ni mchanganyiko wa fedha, madaraka, tamaa, usaliti, visasi na mapenzi ambayo huwa ni sehemu ya chanzo cha yote hayo.

Professor Bili ni bingwa wa kupiga hesabu zake huku akiwatumia watu mbalimbali katika michezo yake michafu. Mpambe wake Thomas, moja ya wanafunzi wake vipanga ambaye pia anakubalika sana katika jamii anatumika kufungua shirika la kusaidia yatima na walemavu.  Mwanzoni wanaliendesha vizuri shirika hilo hadi pale Michael (Mtoto wa Professor Billi) ambaye alikuwa anajihusisha na mapenzi na mwanafunzi na kisha kumtelekeza alipoajiriwa na shirika hilo. Thomas naye alipoona kama anatumiwa na Bili anaamua kulipiza kisasi kwa kuanza mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa kufikia wa Billi.

Mambo yanavurugika pale mapenzi, fedha na tamaa yanapotawala katika kisa hiki mwanana cha Jua Kali.