Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Karembo amerudi – Pazia

Habari
15 Juni 2021
Baada ya Bidu kudhani kwamba amempata Tunu tena, ghafra Karembo arudi tena.
Untitled design (26)

Kipindi Bid una Tunu walivyokuwa kwenye ndoa kasheshe nyingi ziliwakumba. Kuanzia kwa Tunu kumsingizia Bidu kwamba alimbaka Regina na pia pia Tunu kumletea Bidu madeni. Ndoa yao ilikuwa mashakani na Bidu aliamua kuachana na Tunu na kumpa talaka tatu. Kwa dini ya Kiisilamu mwanamume akimpa mwanamke talaka tatu maana yake ndoa ndio imeikwisha kabisa na hamna njinsi yeyote ya kuiokoa.

Baada ya kumpa Tunu talaka, moyo wa Bidu ulimuuma sana. Siku moja alimua kwenda club na alivyokuwepo huko akakutana na Karembo. Baada ya kunywa na kula mpaka Bidu kupoteza fahamu aliamkia gesti na Karembo. Karembo akamwambia kwamba walifanya mambo na sasa ana hisi kwamba anaweza kuwa na mimba. Ikabidi Bidu ampesa ili aende kutoa mimba na aachane nae.

Kurudi nyumbani, Bidu aligundua kwamba Tunu alikuwa amesha chumbiwa na Sadiq na walikuwa wanapanga ndoa yao. Baada ya ndoa Bidu alijiona kwamba amekosa mke wake milele na akanza kufanya yote ili warudiane.

Bahati nzuri, Tunu alikuwa mjamzito na iligundulika kwamba ujauzito wake ulikuwepo kabla ya kuolewa na Sadiq. Maana yake kama kwa mila za kiisilamu Tunu sio mke wah alali wa Sadiq ila bado ni mke wa Bidu.

Baada ya kurudi nyumbani, Karembo alikuja kwa Bidu kudai kwamba ana mimba na kwamba Bidu alimbaka. Hili jambo lilimuumiza Tunu na hajui kama akae na Bidu au arudi nyumbani.

Fuatilia kipindi cha #MMBPazia kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 1:30 usiku kugundua zaidi.