Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Gloria na Eliza wagombania Henry - Pazia

Habari
22 Aprili 2021
Eliza agundua kwamba mwanamke mpya kwenye maisha ya Henry ni mwanae Gloria.
Screenshot 2021 04 22 at 15

Eliza alishawahikuwa na mahusiano na Henry miaka 20 iliyopita, waliachana baada ya kukutana na Mariam, Henry aliamua kuachana na Eliza. Tendo hilo lilimuumiza Eliza sana kwasababu bado alikuwa anampenda Henry.

Baada ya miaka 20 kupita, Eliza akutana na Henry tena, wote wameshakuwa watuwazima na washepata watoto na wameshatulia kimaisha. Eliza aliona kwamba ndio muda sahii kurudiana na Henry. Kwa Eliza tatizo, ni Miriam, muda wote akimkosa Henry alikuwa akidhani kwamba ni kwasababu alirudiana na Miriam.

Hatimaye, Eliza aligundua kwamba Henry anamwanamke mpya, na huyu mwnamke sio Miriam. Baada ya upelelezi, aligundua kwamba huyu mwanamke mpya ndani ya Maisha ya Henry, ni mwanae Gloria. Gloria alikuwa anatembea na Henry kama sugardaddy wake wakati akijua kwamba mama yake na Henry walalishawahi kuwa wapenzi.

Je unafikiri Eliza atamsamehe mwanae? Usikose kuangalia #MMBPazia kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku.