Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Fred amtaka Brenda - Pazia

Habari
21 Juni 2021
Fred aweka hisia zake wazi kuhusu Brenda.
Screenshot 2021 06 21 at 13

Kipindi Brenda alivyohamia mjini, Fred alisema kwamba Brenda ni mdogo wake lakini ukweli ni kwamba walikuwa marafiki tangu walivyokuwa wadogo. Kwasababu hawakuwa na familia zao karibu, wlifanikiwa kuwa karibu sana.

Alivyofika chuoni, Brenda alikutana na Ben. Ben ni mwanamuziki na Brenda alianza kumdhamini kwenye kazi yake ya muziki. Mwanzoni mahusiano kati ya Ben na Brenda yalikuwa ya kibiashara tuu lakini baadae mahusiano yao yalibadirika kuwa yakimapenzi.  Fred alivyoona ukaribu wao alikasirika sana, alikasirika kwasababu alikuwa akifikiri kwamba Ben alikuwa anamtumia Brenda kwa pesa zake.

Baada ya kugundua kwamba ni kweli Ben alikuwa anamtapeli Brenda, Fred alijaribu kumwambia Brenda na Brenda hakumsikiliza. Baada ya Brenda kukataa kuachana na Ben, Fred aapa kumpata kimapenzi kwasababu siri yake muda wote ni kwamba alikuwa anampenda Brenda na kwamba wazazi wake wakuwa wanataka Fred na Brenda waoane. Je Fred atafanikiwa kumpata Brenda?

Usikose kuangalia #MMBPazia kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 1:30 na pia kumbuka kwamba unaweza kuangalia msimu mzima wa Pazia kwa njia ya DStv Now.