Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Eliza ataka kulipiza kisasi – Pazia

Habari
20 Julai 2021
Eliza amekasirika na anataka kila mtu aliyemkosea alipe.
Screenshot 2021 07 20 at 10

Baada ya kugundua kwamba mwanae, Gloria alikuwa anatembea na mchumba wake wa zamani Henry, Eliza anahisi kwamba hamna mtu yeyote ambaye anaweza kumuamiani. Aamua kuandika orodha ya watu ambao hawaamini na jinsi gani atawlipza kisasi kwa yote waliyomfanyia.

 

  1. Henry

Ingawa Henry anajua kwamba Eliza alikuwa anampenda, aliendelea kuwa na mahusiano na mtoto wake na Eliza, Gloria. Harafu pia, Henry aliendelea kumtaka Mariam, mama yake na Regina. Eliza alichofanya ni kumuonyesha Henry kwamba Mariam alikuwa na mahusiano na bosi wake na pia kumwambia Henry kwamba Gloria ni mwanae.

  1. Mariam

Eliza anawivu na Mariam baada ya Henry kuendelea kumpenda Mariam kuzidi Eliza. Eliza aamua kuwaonyesha Regina na Henry kwamba Mariam alikuwa anatembea na bosi wake na kwamba aliamua kuachana na familia yake juu ya bosi wake ili Henry na Regina wamkasirikie.

 

  1. Regina

Tatizo kubwa Eliza alilokuwa nalo na Regina ni kwamba alitoa pesa kwa Henry ili Regina aende shule na Regina alikataa kusoma na alibeba mimba.

 

  1. Gloria

Eliza anafikiri kati ya wote, Gloria ndiye aliyemzaliti kuzidi. Baada ya miaka nenda rudi ya Gloria kuona jinsi mama yake alivyompenda Henry, bado kama mwanae alienda kuanza mapenzi na Henry. Kumuumiza Gloria alimwambia kwamba Henry ni baba yake.

 

Eliza ameapa kulipiza kisasi kati ya hawa watu wanne ni nani kati yao anastahiri zaidi kulipizwa kisasi? Usikose kuangalia #MMBPazia kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 1:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.