Logo
MMB PaziaSM TwitterCover
channel logo dark

Pazia

160Tamthilia13

Bidu anataka kurudianan na mke wake – Pazia

Habari
26 Mei 2021
Baada ya Tunu kuolewa na Sadiq, Bidu amtaka tena.
Untitled design (27)

 

Mahusiano kati ya Bidu na Tunu hayakuwa mazuri. Baada ya Tunu kumsingizia Bidu kwamba ndiye aliyembaka Regina, Bidu aliomba talaka. Kwa jinsi alivyoomba talaka ilikuwa kwa sababu alikuwa amekasirika na kwasababu Tunu alikuwa anataka kuishi Maisha ya kifahari wakati hakuwa na pesa.

Wakati huo, Tunu alianza kudai kwamba amebeba mimba, na aliamua kumwambia Bidu kwamba mimba ni ya Sadiq, wakati Bidu alivyokuwa jela. Hili jambo lilimfanya Bidu asisitize kupata talak ana hatimaye waliachana.

Baada ya talaka, Tunu aliamua kumuoa Saqik. Bidu alihudhuria harusi lakini moyo wake ulimuuma sana, nah apo ndipo alipoanza kujuta uamuzi aliyofanya.

Alirudi chumbani kwa Tunu kujaribu kumchukua lakini hakupewa ruhusa. Baada ya muda, Bidu aliamua kwenda kuongea na Sadiq ili amuone Tunu lakini Sadiq alimkatalia. Bidu anajuta sana baada ya kumwacha Tunu, je unafikiri ataweza kumpata tena? Fuatilia #MMBPazia kila Jumatatu hadi Jumatano ndani ya DSTV chaneli 160 kugundua.