Logo
NYAVU
channel logo dark

Nyavu

160Drama16

Pande Mbili za Grace Mapunda – Nyavu

Habari
12 Oktoba 2020
Kipenzi wa washabiki wa Maisha Magic Bongo, Grace Mapunda amefanikiwa kuigiza kama Tesa ndani ya #HubaTZ na pia kama Shani ndani #NyavuTZ.
Grace Mapunda Article

Kazi mbili lakini, nyota moja inayo angaza! Grace Mapunda anakipaji kikubwa na kinaoneakana kwa jinsi alivyoweza kuigiza ndani ya vipindi hivi tofauti kabisa na majukumu tofauti ndani ya Maisha Magic Bongo. Kwenye #HubaTZ, Grace panaigiza kama Tesa, ambaye ni mkali na aliye tajiri sana. Tesa ni mama yake Devi, na Tesa pia ndiye mtu aliye muua baba yake Devi akitaka kurithi mali zake. Baada ya kuwa mjane Tesa akanza na tabia ya kutembea na wavulana wadogo kama ‘sugar mama’. Kwa sasa hivi, Tesa ana mahusiano na Hank. Hank alikuwa anampenda sana Tesa lakini siku hizi macho yake yote yameamia kwa Aneth.

Kwa upande mwingine wa #NyavuTZ Grace anaigiza kama Shani. Shani ni mfanya kazi wa ndani nyumbani kwa Lena na Heri. Shani ni mnyenyekevu na ni masikini ukilinganisha na Tesa. Shani hana watoto, lakini Stoni ana wasiwasi kwamba Shani ndiye mama yake wa kumzaa, na walimnyanganya mwanae alivyo zaliwa. Shani amejikuta kwenye tabu na Siti, na hili tatizo linaweza kumletea kifo – kwani huu ndio utakuwa mwisho wa Shani?

Usikose kuangalia #HubaTZ kila Jumatatu mpaka Ijumaa saa 3 usiku na #NyavuTZ Jumatatu hadi Jumatano saa 1:30 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo, chaneli 160.