Logo
Nyavu Slim BB
channel logo dark

Nyavu

160Drama16

Show jipya yaja mwezi huu katika MMBongo - Nyavu

Habari
05 Mei 2020
Tamthilia za kipekee zinazinduliwa hapa MMBongo! Pata simulizi penzi ya NYAVU, kila Jumatatu hadi Jumatano saa 1.30 usiku!
<p>Nyavu launch article</p>

Wahenga walisema hivi: “akili isiyo na utulivu ni warsha ya Shetani”. Fifi aligundua jambo hili baada ya kumaliza masomo yake katika shule ya upili.

Alijipata akiwa na muda ya ziada ambayo alitumia kupitia pitia ukuraza za mitandao ya kijamii. Akiwa pale akakutana na ‘Shetani’ mwenyewe aliyejulikana kama Ston lakini kwake alikuwa anajulikana kama Shafi.

Fifi akaanguka katika nyavu ya Shafi na kuenda naye deti, akiamini kwamba amepata kipenzi wa dhati. Wakati jua lilipambazuka siku ifuatayo, Fifi alijipata kitandani ya hoteli peke yake akiwa amepoteza fahamu kuhusu matukio ya usiku uliopita.

Alipojaribu kukusanya kumbukumbu ya matukuio ya usiku iliyopita, akaona picha ya Shafi kwenye gazeti ya siku. Alitambulishwa gazetini kama Ston na kwamba alikuwa mume wa mtu na mtoto wa pekee wa mmoja ya familia tajiri mjini huo.

Kwa kuongezea, familia yake ina historia ya kuwa wana haramu, hasa mama yake, Ida ambaye ana umashuhuri wa kuendesha biashara bandia.

Utafiti wake wa kujua ukweli kuhusu matukio ya usiku ule walikukana na Ston unafichua mambo mengi zaidi kuliko kile alicho tarajia.

Nyavu inazinduliwa katika Maisha Magic Bongo tarehe 4 Mei 2020 saa 1.30 usiku!  Usikose!