Logo
Nyavu Slim BB
channel logo dark

Nyavu

160Drama16

Bwana Shaka's apoteza kila kitu – Nyavu

Habari
28 Septemba 2020
Tumeangalia jinsi Bwana Shaka alivyoanguka kwenye maisha; je huu ni mlima naoweza kupanda au atizidi kudidmia?
IMG 20200928 141048

Washabiki wa #NyavuTZ walimpenda sana Bwana Shaka walivyokutana naye mwanzoni. Alionekama kama mwanaume mstaarabu, anaye mpenda sana mke wake Ida. Alivyokutana na Ida, Ida alikuwa ameshamzaa Fifi. Bwana Shaka alimpenda sana akaamuoa Ida harafu akamlea Fifi kama mwanae.

Baada ya ndoa, familia ilizidi kuongezeka na wakazaa mwanao wa kiume, Sudi. Vitu vikaanza kuenda vizuri kwa familia ya Bwana Shaka – na watu wakamsifu Bwana Shaka, wa kumlea Fifi kama mtoto wake aliyemzaa.

Vitu vilianza kwenda vibaya ndani ya nyumba ya Bwana Shaka, Fifi alivyotekwa na akapotea.  Ndani ya kipindi hicho, Bwana Shaka, alijifunza kwamba Ida na bosi wake, Bwana Heri, walishawahi kuwa wapenzi. Na pia kwamba Fifi alikuwa ni mtoto wa Bwana Heri. Hilo swala lilimuumiza sana Bwana Shaka. Akanza kuona hata wivu kwa jinsi Bwana Heri alivyokuwa tajiri na alihisi kwamba, Bwana Heri bado anampenda Ida. Kilicho muumiza zaidi, ni kwamba Ida alimlimbilia Bwana Heri kwa msahada Fifi alivyopotea na Bwana Shaka akanza kufikiri kwamba Ida na Bwana Heri watarudiana.()


Fifi alivyopatikana akaanza kuwa karibu na baba yake mzani, Bwana Heri. Hapo ndio Bwana Shaka akaumia zaidi, akabidi amtafute mke wake Bwana Heri, Lena, iliamsahidie kurudisha familia yake. Lena anajulikana kuwana roho mbaya na mipango haikuenda sawa, kitu ambacho kilimufanya Bwana Shaka akimbilie kunywa pombe sana. Polepole, vitu vikaendelea vibaya na, Bwana Shaka akazidi kunywa sana na aka achana na Idana kuwatimua watoto nyumbani na pia kuuza nyumba ya familia.

Je Bwana Shaka anaweza kuacha pombe na kuanza kujenga familia yake tena? Usikose kuangalia #NyavuTZ kila Jumatatu mpaka Jumatano saa 1:30 chaneli, 160 ndani Maisha Magic Bongo.