Watazamaji wetu wapendwa wamekuwa wakiuliza kwa muda mrefu lini msimu wa pili wa #MMBNuru utaanza tena hatimaye subira inaisha. tamthilia ya Nuru inahusu ndugu wawili waliochukiana wanajikuta lazima waungane kupambana na adui anaewatandia giza nene maishani mwao, baba yao. Hapo chini ni matukio wakubwa yaliyotokea ndani ya msimu wa kwanza:
Mahusiano ya Ritha na Ronald
Baada ya kugundua kwamba Ritha alikuwa akicheat na Adrian, Ronald alianza mahusiano yake pembeni lakini aliamua kumsamehe Ritha. Baada ya Naomi kumkuta John na Alice, pacha wake wa kufanana na Ritha, alimwambia Adrian. Sasa Adrian alibaki kudhani kwamba Ritha alirudia kumcheat, Ronald aliamua kufanya maisha kivyake wakati muda wote mtu aliyedhani ni Ritha alikuwa pacha wake Alice.
Adrian na Naomi
Baada ya kushindwa kupata kampuni ya Mzee Andrew, Adriam aliamaua kujaribu kumtongoza Naomi.
Mzee Andrew na Juliana
Baada ya Jualiana kukutana na Mzee Andrew aliacha na mama yake aliyekuwa kimtesa na alihamia kwa Mzee Andrew lakini anasiri kubwa ya Adrian.
Alice agundua kwamba ana pacha
Baada ya Ritha kumgundua Alice na kumleta ofisini, Alice agundua kwamba Ritha anaweza kuwa pacha wake aliyepotea zamani.
Danny na mke wake
Baada ya kukataliwa na Jualiana Danny aliamua kufanya bidi nyumbani lakini mke wake amekuwa akimroga.
Ronald na Doreen
Baada ya Ronald kuanza mahusiano na Doreen, watazamaji waligundua kwamba Doreen amekuwa akimtapeli Ronald na msimu uliopita alidai kwamba ana ujauzito.
Ni nani unahamu zaidi ya kumuona ndani ya msimu wa pili wa #MMBNuru.
Usikose vipindi vipya kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku ndani ya MaishaMagicBongo.
Pata kujua waigizaji wa tamthilia hii hapa: