Logo
Nuru
channel logo dark

Nuru

160Drama16

Nuru: Hitaji la Moyo - Maisha Magic Bongo

Habari
01 Februari 2024
Mzozo wa Familia na Vita vya Biashara
Article

Mr. Andrew Mapambano 65. mfanyabiashara mkubwa mwenye mtoto mmoja wa kike aitwaye Naomi 28 pia anaishi na Adrian ambaye ni kijana aliyekuwa amemuajiri kama shambaboy wake ambaye alitokea kumuamini sana na kumsomesha na baadaye kumpa ajira kama msaidizi wake wa karibu kwenye kampuni. Andrew ana matamanio ya kumfanya Naomi kuwa bora kuliko Adrian lakini yanashindakana kutokana na vikwazo vinavyowekwa na Adrian vya kumshusha Naomi mbele ya macho ya Andrew ili Adrian aendelee kuwa bora machoni kwa Andrew. Andrew anajikuta akimdharau mwanae Naomi pasipo kufahamu kwamba vikwazo vya kushindwa kwake vinawekwa na kijana Adrian ambaye Andrew anamuamini kupita kiasi. Naomi anaingia kwenye migogoro mizito na Baba yake Mr. Andrew bila kujua yote hayo yamesababishwa na Adrian.

Andrew hapendi kuona kijana aliyemlea anakuwa juu kuliko mwanae wa kumzaa lakini anakosa cha kufanya kutokana na kumuona Naomi hawezi kufaulu yale anayoyahitaji. Mambo yanaanza kubadilika baada ya Andrew kuambiwa na hawara yake Bi. Marry ambaye ni mke wa rafiki wa karibu kabisa wa Andrew kwamba mtoto Ronald 33 ambaye ni mtoto wa ndani ya ndoa ya Marry na Mr. Mashao (Mume wa Marry na rafiki wa karibu wa Andrew) ni mtoto wa Andrew. Andrew anapoyafahamu hayo haichukui muda mrefu Mr. Mashao anamuua Bi. Marry na kujiua baada ya Mr. Mashau kugundua Marry anamsaliti na Ronald ni mtoto wa Andrew. Andrew anampa mamlaka makubwa Ronald ofisini na kumshusha cheo Adrian huku akimuonesha Ronald upendo wote kama mzazi wake bila ya Ronald kufahamu kama Andrew ndiye Baba yake mzazi aliyesababisha vifo vya wazazi wake. Ronald anatamani kumfahamu mtu huyo aliyekuwa na urafiki wa karibu na Baba yake ili amlipizie kisasi lakini inabaki kuwa siri ya Mr. Andrew. Kuna ibuka vita kubwa sana ya kimaslahi kati ya Adrian na Ronald, kwani licha ya mambo ya kikazi, Adrian anatembea na mke wake Ronald anaeitwa Ritha.

Usipitwe na vipindi vya #MMBNuru kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku ndani ya DStv chaneli 160!