Logo
Nuru
channel logo dark

Nuru

160Drama16

Kutana na Nyota za #MMBNuru: Hadithi za Mapambano, Upendo, na Siri

Habari
22 Februari 2024
Pata fursa ya kutambulishwa na waigizaji wa kipindi cha #MMBNuru
Nuru

Hawa ndio wahusika wanaojenga hadithi ya kusisimua na ya kipekee katika ulimwengu wa tamthilia ya kusisimua, wakiweka msingi wa mapambano, upendo, na utambuzi. Wanaonyesha jinsi maisha yanavyoweza kuwa na changamoto na furaha, na jinsi ya kuvuka mipaka yake. Tutazame jinsi hadithi yao inavyokua na kushirikisha hisia zetu na uzoefu wetu wenyewe.

Wahusika Wakuu:

Mr. Andrew (65)

Mtu mwenye hasira za haraka, lakini pia na siri zisizotarajiwa. Anaonekana kama mtu wa utajiri na mamlaka, lakini kuna mengi zaidi nyuma ya pazia lake. Anajikuta katika penzi zito na Juliana, binti wa uswahilini, na kutumbukia katika mizozo mikubwa kati ya wahusika wengine.

Naomi (28)

Msichana mpole lakini mwenye hisia kali, anayepambana na changamoto za kuweka alama yake katika maisha ya baba yake, Mr. Andrew. Anaishi chini ya kivuli cha mdogo wake wa kufanya kazi, Adrian, na hujitahidi kupata heshima na upendo kutoka kwake.

 

Adrian (33)

Mtu mnafiki na mwenye kiburi, ambaye uchu wake wa kutawala hufichwa nyuma ya tabasamu la kuvutia. Anayewakandamiza wengine ili kutunukiwa na kupendwa na Mr. Andrew, na kujikuta katika ugomvi mkali na Ronald.

 

Ronald (33)

Kijana mpole mwenye hisia kali, ambaye maisha yake yamejaa changamoto na uamuzi mgumu. Anapambana na upendo na uaminifu, akipigania mahali pa heshima katika familia ya Mr. Andrew na kukabiliana na vita na Adrian.

 

Ritha (30)

Mwanamke mrembo anayependa kujilipiza kisasi, anayejaribu kudumisha uhusiano na mume wake huku akiingia katika mapambano ya moyo na usaliti.

 

John (33)

Kijana aliyejeruhiwa kihemko, anayependa wanawake lakini akijikuta katika matatizo ya moyo. Kuingia kwake katika mahusiano na Naomi na Alice kunazua machafuko makubwa katika maisha yake.

 

Alice (30)

Binti mrembo na mwenye nguvu, ambaye anajikuta katika mapambano ya ndani ya moyo na mapenzi. Anapambana na uaminifu na kujaribu kuelewa hisia zake.

 

Juliana (28)

Msichana wa uswahilini mrembo ambaye anajaribu kuepuka kufanyishwa kazi za uganga wa kienyeji bila ridhaa yake. Anaingia katika mahusiano na Mr. Andrew na kugundua uovu wa Adrian.

 

Wahusika Wasaidizi:

Bi. Anna

Mama mkubwa wa Juliana, anayejitambulisha kama mganga feki wa kienyeji.

Bi. Teddy

Mama wa Alice, ambaye amepooza kitandani.

Danny

Kijana fundi gereji wa uswahilini ambaye amependa Juliana.

Doreen

Mfanyakazi wa Andrew ambaye anaingia katika uhusiano wa kutatanisha na Ronald kwa ajili ya kulipiza kisasi.

Maganga

Baba aliyekutana na Alice na kumtaka kimapenzi lakini numbani ana mke na ana ugonjwa wa ukimwi.

Mama G

Mke wa Maganga na anaujauzito wake.

Deus

Rafiki wa karibu wa John, wanafanya kazi pamoja.

 

Kumbuka kufuatilia kipindi cha #MMBNuru kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 4 usiku ndani ya DStv chaneli 160, pia jiunganishe na #MyDStv App au fuatilia tovuti ya DStv kuangalia popote ulipo.