Logo
channel logo dark

Mzooka

160MusicalPG13

Taarifa na Video moto moto hapa Mzooka!

Habari
06 Juni 2018
Ni yapi mazuri na mapya katika ulimwengu wa muziki na burudani? SOMA ZAIDI!
<p>Screen Shot 2018-06-06 at 15.37.18</p>

Hapa MMBongo tunakata anga za burudani kwa kugusa sekta mbali mbali za burudani,  na tukiongelea burudani hatuwezi kuuwaacha nyuma Mastaa wetu! Je, wamejishughlisha na nini wiki zilizopita? Ni yapi mapya katika ulimwengu wa burudani na Sanaa? Na vipi kuhusu kurasa zetu za kijamii?

Huko Instagram wasafi wameuwasha moto! Je, ni kweli Diamond na Zari wanarudiana?

Wasafi Records wako kazini! Wanaangusha singles moto moto mfululizo , ni kama maji ya mfereji! Na kwa kweli, zinakata kiu ya muziki murwa, bongo fleva taslimu, beats zao zikimtoa nyoka pangoni!

Harmonize na Diamond Platnumz wametuletea kibao kipya ‘Kwangwaru’ collabo yao ikiwa ya kipekee!

Single mpya kabisa, Diamond anashirikiana na Rayvanny katika single “Iyena’. Je, kati ya Rayvanny na Harmonize nani mkali kati yao?

Halkadhalika, msanii wa  hiphop, ZaIID amepiga tour yake kali kote nchini akiwa na hit single yake  “Wowowo’ iliyotolewa mwezi wa Agosti 2017. Ameahidi mashabik wake ngoma zingine kali hivi karibuni.

Pata video za ngoma kali na taarifa nyingi mbali mbali kila kila Jumatatu=-Ijumaa saa 10 jioni katika kipindi cha Mzooka!