Staa wa muziki kutokea kwenye Bongo Fleva Ali Kiba aliyewahi kuwa na mahusiano ya muda mrefu na Jokate ni dhahiri fununu za mahusiano yao kuisha ni kweli kabisa.
Ali Kiba ameamua kuvuta jiko Mombasa nchini Kenya April 19,2018 ambapo kafunga ndoa rasmi na mke wake Amina Khalef Ahmed. Maharusi hawa walifunga ndoa katika msikiti wa Ummul Kulthum na baadaye sherehe za Ukumbi au reception zinatarajiwa kufanyika Dar Es Salaam.
Hizi ni baadhi ya picha za kinachoendelea Mombasa katika harusi hiyo.
Katika habari zingine kutoka ulimwengu wa sanaa, wanamuziki mashuhuri Diamond Platnumz (Nasib Abdul) na muimbaji Nandy (Faustina Charles) walitiwa mbaroni kutokana na video walizopeperusha katika mitambo ya ya intaneti.
Kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi kulitokana na amri ilityotolewa na raisi wa Jamuhuri ya Muungano Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuhusu wajibu wa kila mtanzania katika matumizi ya mitandao kwa makini. Nasib na Faustina walilipa dhamana bila mashtaka mahakamani na kuwachiliwa Jumatatu iliyopita.
Kupata video mpya na habari za wasanii wa Bongo, tazama Mzooka, kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 jioni hapa #MMBongo! Ni Yetu!