Logo
Mzooka slim New
channel logo dark

Mzooka

160MusicalPG13

WCW wiki hii, Lady Jaydee na single mpya, Baby.

Habari
17 Januari 2018
Leo kama Jumatano, ni wakati wa kuwaletea mashabiki wa #MzookaTZ WCW wa wiki hii!
Lady Jaydee 2

Judith Wambura Mbibo ajulikanaye kama Lady Jaydee ni msanii kikongwe kutoka Tanzania. Binti anayejulikana bara la Afrika na kote duniani, Lady Jaydee ametoa single murwa mpya iitwayo “Baby’.

Lady Jaydee amesajiliwa na label ya Taurus Muzik na ndiye muimbaji wa nyimbo kama ‘Ndindindi’, ‘Joto Hasira’ na ‘I miss you’. Nyota ya Lady Jaydee inapepea akiwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kuimba nyimbo za ‘Rhythm & Blues (R&B) katika lugha ya Kiswahili. Ameshirikiana na wasanii vikongwe kutoka bara la Afrika kama mwimbaji maarufu, Salif Keita kutoka Mali, Kidum kutoka Burundi na Joh Makini, mwana wa Tanzania.

Msanii nyota Jaydee ameshinda tuzo kadha wa kadha kama East Africa TV Awards, Africa Magazine Muzik Awards na All Africa Music Awards. Kweli Lady Jaydee anafaa jina lake likiwa “Malkia wa Bongo Fleva”.

Pata single mpya ‘Baby’ hapa na usikose kujiunga nasi kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 jioni katika kipindi cha Mzooka kupitia DStv chaneli 160 ikiwa Maisha Magic Bongo! Ni Yetu!