WCB Wasafi Records wamtambulisha Mbosso kwenye label yao ya WCB siku mbili zilizopita. Mbosso alikua miongoni wa wasanii waliokuwa kwenye kundi la Yamoto Bendi na kwa sasa, kundi hilo halipo tena kila mmoja anafanya kazi kwa kujitegemea.
Lakini, katika shughuli hii ya kumualika Mbosso kwenye lebo ya WCB, walialikwa watu wengi ila kuna mgeni mmoja ambaye alifanya watu wazungumze sana. Mgeni huyo alikua mwigizaji maarufu, Wema Sepetu amabaye anajulikana kama mpenzi wa zamani wa Diamond Platnumz na kwa maneno mengine walikua Super couple iliyotikisa Tanzania. Uwepo wa Wema Sepetu ulikuwa na maswali, lakini, kilichofanya watu waongee sana ni pozi walizokuwa nazo yeye na Diamond Plutnumz mikao yao kwa kweli ulikua na maswali mengi sana!
Wema alisema amepeta mualiko kutoka kwa Diamond, na ni Diamond mwenyewe ndiye aliyempigia simu kumualika katika hiyo shughuli yao. Anaongeza akiwapa pongezi kubwa Diamond na timu yake yote kwa kiukweli ndoto zake zimetimia. Kwa sasa, hamna utafauti wowote kati yao bali kwa sasa wamekuwa ni marafiki wazuri tu, alisema Diamond.
Akimalizia, Diamond katika posti zake za instagram alisema kama aliye shabiki yake wa kweli basi huwezi kufurahia yeye akiwa na ugomvi na mtu yoyote na yeye na Wema wameshamaliza tofauti zao.
Kutana na Diamond na kundi la wasanii wote wa WCB katika Mzooka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 Jioni kupitia Dstv160 Pekee.