Logo
MMB MWALI HDTV

Wajue mastaa ndani ya  Mwali – Maisha Magic Bongo

Habari
27 Oktoba 2022
Fahamu nani ni nani ndani ya Mwali!
Untitled design (1)

Kipindi   cha #MMBMwali kinatarajia kuanza ndani ya DStv chaneli 160, Jumamosi hii, tarehe 29 Oktoba. Acha tuwatambulishe waigizaji wa tamthilia hii.

MWALI

Mwalimindu binti wa Chifu Kandamsile, Msomi, mwerevu na jasiri anetumbukia katika mapenzi mazito  yatakayo jenga  au kubomoa na Nozo , Mwali anapenda sana familia yake n ani  kila kitu kwake and  hasira sana lakini mwepesi wa kusamehe. Mwali anapenda utawala wa haki ni kiongozi wa harakati za muungano.

NOZO

Nozo ni mtoto wa Chifu Pingu, anaezama penzini na Mwalimindu binti wa Kandamsile pia yeye ni msomo mpenda watu hususan familia yake. Nozo anajishughulisha na uvuvi na Hodari sana wa kupiga zumari , sio mwepesi wa hasira kamaalivyo mpenzi wake mwali ila ana maamuzi ya haraka sana. Hapendezwi na tabia za baba yake na mfumo wake wa utawala wake.

SEMINDU

Semindu ni mtoto wa kambo wa Chifu Kandamsile, hakufanikiwa kupata elimu kama wenzake. Semindu ni mkorofi na mtu mwenye hasira na chuki mara nyingi. Anapenda madaraka na kuheshimiwa, anafanya maovu ili kupata anachokitaka.

ZAWADI

Zawadi ni binti wa Mzee Haji Rafiki yake mkubwa Mwanahawa, ana alipata nafasi ya kupata elimu  kwasababu ya utawala wa Chifu pingu na unyayapaaji wake hakuweza kumaliza elimu yake  . Ni binti  mwenye hasira sana na kiu ya kisasi kwa familia ya Chifu Pingu. Anampenda sana Nozo na yupo radhi kufanya chochote ilimradi tu ampate Nozo.

TAUSI

Tausini binti wa Chifu Pingu na mdogo wake na kipenzi cha  Nozo ni mwanafunzi binti mwadilifu, anaamini katika penzi la kaka yake  na Mwali. Tausi ni mtu anapenda haki na kupinga mila kandamizi kwa wanawake. Pia ni mpenzi wa kuchora, ni muumini mkubwa wa muungano.

CHIFU KANDAMSILE

Chifu Kandamsile ni mtawala wa Boma la Kandamsile na baba yake Mwalimindu. Ni baba mkali sana mwenye gadhabu muda mwingi na anatawala kwa mabavu na hapendi kushauriwa. Ni mnyanyasaji na mnyonyaji kwa Watawaliwa. Chifu Kandamsile ni mpenzi wa kula nyama pori, matunda pori na maziwa. Anampenda sana binti yake Mwali kiasi cha kumtaka awe mrithi wa kiti chake  lakini pia hataki muungano.

CHIFU PINGU

Chifu ni mtawala wa Boma la Pingu. Hana sauti kubwa Kiutawala, Hajali kuhusu familia. Ni dhaifu kwa Wanawake hasa Kimapenzi. Anapenda kuvuta tumbaku kwa kiko na starehe yake ni Mapenzi. Hana msimamo katika harakati za Muungano.

JEFA

Jefa ni kijana jasiri na shupavu, kazi yake kubwa uwindaji. Anampenda sana Mwali akiwa akiamini kwamba ni fungu lake la ndoa. Anataka kuwa mtawala kupitia ndoa yake na Mwali. Yuko radhi kufanya lolote lilie aweze kupata penzi la Mwali.

MZEE HAJI

Mzee Haji ni Rafiki, mshauri mkuu wa Chifu Pingu, na baba yake na Zawadi. Anasimama  kama kivuli cha mtawala kwenye Boma. Anampenda sana binti yake, Zawadi, na kila anachokifanya anaweka maslahi ya binti yake mbele.

MZEE MTAMA

Mzee Mtama ni tabibu, mtabiri, na mwanaharakati wa maendeleo ya jamii na usawa. Anaamini mapenzi ya Nozo na Mwali yanaweza kuwa suluhu ya uadui kati ya Boma la Pingu na Kandamsile. Na ni mlezi na nahodha wa harakati za muungano.

MWANAHAWA

Mwanahawa ni mdogo wake mke wa Chifu Pingu na ana chuki na kisasi dhidi ya dada yake. Hana mapenzi ya kweli kwa mtu yeyote. Amemnasa Chifu Pingu Penzini kama sehemu ya kisasi kwa dada yake na siyo rafiki mwaminifu kwa Zawadi.

Usikose kuangalia #MMBMwali kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo!