Logo
Mizani
channel logo dark

Mizani Ya Ushambenga

160UhalisiaPG13

Wanaume wanaovutia katika MMBongo!

Habari
29 Juni 2018
Wanaume wa MMBongo wanatisha kweli! Ni yupi anayefanya damu ikakimbia kwako? SOMA ZAIDI kisha tupe uhondo!
<p>MMB - June Billboard Image 1600 x 640</p>

 Hapa Maisha Magic Bongo, tungependa sana kuwashukuru na kuwapa pongenzi ndugu zetu wasanii na waigizaji, wanaume wetu wenye mvuto Zaidi hapa Maisha Magic Bongo! Bilas haka, vipaji na talanta zao zinatuletea burudani bila kikomo!

Sisi MMB mwezi huu tukaona sio mbaya kama tuta sherehekea wananume wanaopamba na kutmba katika runinga zetu kupitia vipindi mbali mbali na kutufanya tufurahie chaneli ya maisha magic bongo kila siku

Tukiangazia macho katika sekta ya filamu na muziki tunaona  WCB wananvyo jituma kila siku kuhakikisha muziki wao sio tu unapendwa bali untambulika na wenye ubora kote duniani , kuna kina ASLAY, NAVYKENZO, JUX,WEUSI, BARNABA, ALIKIBA na wengine wengi, wanawake pia hawakuachwa nyuma tunaona wengi wakifanya juu chini kusambaza kazi zao hususa wasanii wa kike filamu zetu na tamthilia zina ngara kweli kweli.

Je , ni staa yupi kati ya hawa mashujaa wetu wa MMBongo amewahi kufanya damu isimame au moyo kwenda kasi?

ISHAAN (DOLI ARMANO KI):

Ishaan hatimaye nyota yake inangaa kajipatia jiko naye, ni bibie Urmi aliyekuwa shemeji yake! Samrat anakwazika kusipo kifani, anaungana na mama mkwe wake katika kufarakanisha ndoa ya Ishaan. Je,watafanikiwa?  Kipindi kila Jumatano na Alhamisi saa 12 jioni hapa #MMBongo! 

 

JUDE (HUBA):

Mugizaji mpya katika tamthilia ya HUBA, Jude amejikaanga  na mafuta yake mwenyewe! Anafika na kutakwa na kila mwanamke wa Fuli Gem Stones lakini huba lake lipo kwa Batuli. Kibibi anaweweseka baada ya kugundua mahusiano hayo anafanya juu chini yavunjike Akisimamia kampuni yeye na Roy wakimgoja Dev, ni nini kitaendelea? Jumatatu hadi Jumatano saa 3 usiku! 

 

ASLAY (MZOOKA):

Aslay, msanii chipukizi anayetamba sana katika anga za Bongo fleva kote Afrika Mashariki!  Je, ni kweli kwamba yeye kuondoka Yamoto Band kumemgarisha zaidi? Ngoma! Pata video mpya za Bongo kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 jioni kipindi ni Mzooka!

 

ZUNDE (KITIMTIM):

Zunde au Tin White mvunja mbavu maarufu sana katika tasnia hii ya filamu Tanzania, akishirikiana na bibie Pili na wengine wengi katika Kitimtim! kila Jumatatu saa 1:30 Usiku hapa Maisha Magic Bongo!

 

ROY (HUBA):

HUBA 'Hearthrob' Roy anaendelea kuleta uigizaji wa hali ya juu kwa tamthilia ya HUBA! Roy ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa muda katika Fuli Gem Stones akimngoja Dev. Je Tesa mpenda madaraka atamuacha salama kweli?

MMBongo Hottest men! Ungana nasi kila siku katika juhudi zetu, burudani zisizo na kikomo hapa Maisha Magic Bongo! Kama ilivyo desturi yetu, tunawatakia Ijumaa njema!