Logo
 slim mchikicho new
channel logo dark

Mchikicho Wa Pwani

160RealityPG13

Siri nane kuhusu Bi Mariam Migomba!

Habari
08 Novemba 2018
Mami Originali anafungua roho hapa Maisha Magic Bongo na kutoa mambo nane tusiojua kumhusu! SOMA ZAIDI!
Siri nane kuhusu Bi Mariam Migomba!

Jamii zetu maswala ya kufunda mwali au hata wanaume na miongoni mwa wafundaji wazuri tulionao Tanzania ni  Bi Mariam wa Migomba ni somo,

kungwi kweli kweli! Akigusia mada, tabia ,ushauri na mengine mengi yanayofanyika na kutokea katika maisha yetu ya kila siku  ya KItanzania  

Jumatano ya leo tukaona sii haba kama tumjue Bi Mariam Migomba ni nani? Tumetazama na kumskia akisema mengi katika Mchikicho wa Pwani kwa muda sasa na lengo lake siku zote ni kuelimisha jamii zetu kwa mada zinazo gusa maisha yetu moja kwa moja

Lakini, Bi Migomba ana maisha yake pia , tofauti kabisa na tumuonavyo katika runinga ya Maisha Magic Bongo!

Mambo 10 hatujawahi kujua kuhusu Mami wetu originali!

1. Bi Mariam ni Mama wa Watoto watatu.

2 Mariam anaipenda sana kazi yake! Na hivi ndivyo alivyosema, ‘ Naipenda sana Kazi hii ya kuelimisha jamii, pia najivunia toka mwali wangu wa kwanza mpaka leo, sijawahi kusikia amaachwa na kutokupata mtoto wowote tumebahatika kuzaa.’

3. Mama Originali sio mtu muoga katika kazi wala Maisha . Anajiamini sana katika kijamii yanayomzunguka, hata kwa mfano, ukiwa Boss wake, ukikosea, atakukosoa kwa mapenzi. Bi Mariam ni msikvu na hupokea ushauri kwa wakubwa  na wadogo na pia  kuuliza kama hajui jambo lolote.

4. Katika upande wa uashauri wa ndoa, anajivunia ndoa nyingi kutoka mikoa na Nchi jirani zilkuwa zikiyumba yumba lakini, kupitia hekima na busara aliyojaliwa na           Mungu mwenyezi, ndoa hizo bado ziko imara!

5. Mami Originali aliaanza kazi ya ushauri toka 2003 mpaka leo!

6. Kitu kimoja kinachomuudhi Bi Mariam ni maneno! “Ukiwa na maneno, nakuacha hapo na ukweli nakupatia!”ndio manaa sina makundi ya ajabu

7. Bi Mariam wa Migomba anapenda sana manukato! Alifungua roho na kusema, “ Napenda sana Perfume! Kama nina pesa chakwanza naweza kununua ni  Perfume kwa gharama yoyote!

8. Mariam anapenda zana Saa za mkononi pia. “Napenda saa nzuri na ninaweza nunua saa kwa bei kubwa. Huo ndio ugonjwa wangu!”

Ni kweli tumebahatika sana kuwa na watu kama  Bi Mariam wa Migomba! Endelea kuungana nasi kupitia kipindi cha Mchikicho wa Pwani, kila Jumatano saa 1.00 usiku katika chaneli yako pendwa, Maisha Magic Bongo!