Logo
slim
channel logo dark

Maisha Yangu

160RealityPG13

Taji Liundi — Maisha Yangu

Habari
13 Machi 2020
Anajulikana kama Master T.
taji liundi

Mtangazaji mkongwe Taji Liundi ni mtoto wa kwanza wa George Bakari. Alipoteza wadogo wake wawili akiwa mdogo wakati mamake aliwapa sumu baada ya kutoelewana na babake. Tukio hilo lilifanya familia yake kutawanyika na Taji na babake wakatoka Tanzania na kuelekea ulaya.

Akiwa huko alijifunza kifaransa. Baadaye wakaenda Zambia, Zimbabwe halafu wakarudi Tanzania. Baada ya kuhitimu alijiunga najeshi la kujenga taifa na kujifunza kuongoza, jambo ambalo alifurahia sana. Kwa sababu alikuwa na sauti nzuri, alipewa nafasi katika IPP Media kuwa mtangazaji. Akiwa pale alitoa mapendekezo ya vipindi na tamasha ambazo hazikuwa zimezinduliwa Tanzania.

Baadaye aliweza kuanzisha kipindi cha kuelimisha watu kuhusu ukimwi na hio kazi ilifungua milango mengi zaidi.

Marafiki wake ambao wamepitia mkononi mwake wanasemba kuwa Taji sio mchoyo katika kufundisha.

Kwa sasa yeye ni balozi na mcheshi wa maswala ya kima katika taifa ya Tanzania.