Nini kinakupa Nguvu ktika kazi ya utangazaji?
Dina:Tangu mdogo nilipenda sana maswala ya ubunifu na kujituma mimi mweyewe, hivyo siku nilipo anza kazi hii rasmi nilifanya juu chini kuhakikisha sauti yangu inafika na kuwagusa wengi, na pale nnapo sikia watu wakisema wanapenda vipindi vyangu, wanajifunza na vipindi vyangu nilifarijika na ilinipa nguvu zaidi kila siku.
Umepata maoni gani kutoka mashabiki na wasikilizaji wako?
Dina: wengi husema Nimebadilisha maisha yao japo sii kipesa, lakini sauti yangu imeweza kuzungumza nao kivingine kabisa.
Ulianza lini kupenda utangazaji lini?
Dina: Nikiwa shuleni, niligundua nina kipawa hichi kwani wanafunzi wenzangu walinisikiliza na kunitii kama kiranja wao .
Ulizaliwa wapi?
Dina: nimezaliwa Arusha na huko ndiko Baba na mama walipokutana, lakini baada ya mama kufariki nililazimika kwenda kuishi na baba.
Ni changamoto gani ulizipata ukiwa mdogo?
Dina: Maisha yalikuwa mangumu kweli, kuanzia kwenye kusoma, baba alipambana kweli lakini mambo yalikua magumu, hata chakula ilifikia wakati ni mlo mmoja kwa siku.
Ulikuwa na ndoto gani ukiwa mdogo?
Dina: nikiwa mdogo nilikuwa nawaza kuwa mwanasheria, sijawahi kuwaz kuwa mtangazaji.
Ulifanikiwa vipi kuwa mtangazaji?
Dina: Nakumbuka nilimsindikiza rafiki yangu aliyekuwa na kazi redioni. Ghafla ikageuka kuwa utaratibu wangu. Siku moja akaja Daudi ambaye alikuwa mtangazaji hapo. Katika stori za hapa na pale aliniambia nina sauti ya utangazaji, baadaye akanipeleka Times, akanitambulisha. Jumatatu iliyofuata nilianza kazi rasmi.
Ili kuona stori zingine nyingine kama hizi za kusisimua, tazama Maisha Yangu kila Jumanne saa 3:30 usiku ndani ya DStv 160 pekee!