Logo
madhu
channel logo dark

Madhubala

160DramaPG13

Vita vya RK na Sultan katika Madhubala

Habari
11 Juni 2020
Madhubala alisaidiwa na mama yake RK kuondoka kwa Rk kwenda kuanza maisha yake mapya. akiwa bado anafanya kazi katika seti ya filamu, RK alikuja na kumchukua kwa nguvu na kumpeleka kwake bila ridhaa yake Madhu.
Screenshot 2020 06 11 at 13

Tabia za RK za unyanyasji na jeuri zake ,zinazidi kupamba moto anawashangaza familia nzima kwa alicho mfanyia Madhubala. Jeuri zake zilimfanya amsaliti Madhu na kumtupia maneno ya kejeli madhubala akamuaa kuondoka kurudi kwao.

Wakati huo huo Madhu amerudishwa nyumbani, mahusiano ya RK na Deepali yanafikia mwisho. Kama kawaida, RK alimpa Deepali maneno yaliyojaa dharau mbele ya mume wake. Depali anaaibika sana mbele ya mume wake na familia yote!

Maisha ya kama mume na mke yanaanza tena, RK na Madhu wakienda kwenye hafla kwa pamoja.  Rk anashangazwa na jinisi ambavyo wakati huu, Madhu hamuogopi, wala kushtushwa na ubabe wake tena. Akiwa na tabasamu usoni na heshima yake kwa famillia ikiwa imebaki pale pale.

 Je Madhu atakuwa anapanga kulipiza kisasi au bado ana mapenzi ya dhati kwa mumewe RK? Wana mambo sana hawa! 

Wanapofika uswahilini alipokuwa akiishi na Sultan, Sultan anawaona na kujawa na jazba kumwona Madhu na RK. Kabla hata hajaongea, alwatan RK anaanza kupepeta mdomo wake kwa matusi na kejeli. Sultan anamtolea RK Bastola, Madhubala anaingilia kati, lakini RK,  ili kuonyesha yeye ndio mshindi, anamvuta Madhu na kumuingiza kwenye gari , kisha, wanaondoka. Je huu ndio utakua mwanzo wa vita kati ya Sultan na RK?

Katika maisha yetu ya kila siku tunashuhudia manyayaso katika Ndoa iwe ni mama yako, dada yako au hata jirani. Je ungemshauri afanye nini?

Kufuatilia uhondo, jiunge nasi katika kipindi cha Madhubala, kila Jumatano na Alhamisi, saa 12 jioni hapa Maisha Magic Bongo!

Changia katika mada hii kupitia kurasa zetu za kijamii, Facebook, Twitter na Instagram @maishamagicbongo