Logo
madhu
channel logo dark

Madhubala

160DramaPG13

Utaendeleza ujasiri wako? — Madhubala

Habari
19 Machi 2020
RK amuuliza Madhu.
madhubala

Baada ya kuvurugwa maisha na RK, Madhu anaamua kuendelea na maisha yake. Anarudi kwa kazi yake ya zamani ya ususi. Akiwa kwenye salon, nakutana na Dipali ambaye anamdhalisha. Wakati anatoka kwenda nyumbani, anapata wana habari wakimgojea inje ili wamuhoji kuhusu ususiano wake na RK.

“Kwa sasa kumetengana. Watu hutengana wala sio mapenzi” Madhu awajibu.

Bitujee naye aamua kujiuzulu kama msaidizi wa RK kwa sababu ya vile alivyomtendea Madhu.

Bitu na mamake RK wanaamua kusaidia RK arudiane na Madhu. Bitujee anamtafutia kazi Madhu katika set ya filamu ambayo RK anafanya kazi.

Wanapatana uso kwa uso. Wote wanaonekana kuwa na wakati mgumu kuwa katika ofisi moja lakini wanaamua kuendelea na kazi. RK anazidisha vituko na kumpa Madhu siku tatu pekee awache kazi lakini wapi.

Je mchezo huu utaendelea hadi lini?

Fuatilia Madhubala kila Jumatano na Alhamisi saa 12 jioni ndani ya MMBongo pekee!