Logo
channel logo dark

Kumi Za Wiki

160Muziki13

Vipindi Vipya Ndani Ya Maisha Magic Bongo

Habari
21 Juni 2021
Mwezi wa Julai tunakuletea vipindi viwili vipya ndani ya chaneli ya Maisha Magic Bongo.
Untitled design (41)

Burudani inazidi kuongezeka ndani ya Maisha Magic Bongo na mwezi wa Julai kutaongeza vipindi viwili vipya.

  1. Harusi Yetu

Kipindi cha Harusi Yetu sio kipya na kwa jinsi watazamaji wa Maisha Magic Bongo walivyokuwa wakiomba kipindi hiki kirudi hatimaye wamepata majibu. Msimu huu mpya utakuwa na mtangazaji, Husna Bona. Jitayarishe kuona harusi mpya na za kisasa za halisi ya Kitanzania. Kila harusi itaonyeshwa kuanzia kichen party, sendoff na harusi yenyewe kanisani.

Usikose kuangalia kipindi cha #MMBHarusiYetu kila Alhamisi saa 1:30 usiku ndani ya DStv channel 160!

  1. Sinia

Sinia ni tamthilia mpya ndani ya Maisha Magic Bongo. Hii tamthilia ina husu muingiliano wenye visa vingi vinavyozaa visasi na malumbano makubwa kati ya pande mbili za watu wa maisha ya juu,ya kati na ya chini.Chanzo kikuu cha migongano kinazalishwa na familia ya kitajiri ya Mr. Venus ambaye ni mfanyabiashara tajiri pamoja na mke wake Rose ambaye ni mwanamama mwenye mafanikio makubwa katika fani ya mitindo.

Usikose kuangalia kipindi cha #MMBSinia kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku ndani ya DStv channel 160!

 

Jiunge na Maisha Magic Bongo kuangalia burudani za hali ya juu nchini Tanzania.