Logo

 Msauzi ni ndugu yake na Zunde na Da Zuu – Kitimtim

Habari
15 Juni 2021
Baada ya kuachana na Pili Msauzi alipotea kidogo, na hivi sasa amerudi.
Untitled design (30)

Msimu uliyopita Pili na Zunde walikuwa wakiwa na shida ndani ya ndoa yao. Hili jambo lilimfanya Zunde amfukuze Pili na alijikuta akianza mahusiano na Bwana Msauzi ili Zunde aone wivu na hatimaye warudiane. Na hilo jambo lilifanya Zunde na Pili kurudiana.

Baada ya kurudi nyumbani kwa Zunde, baba yake mdogo Zunde alikuja kuwa tembelea na alivyokuwepo hapo, aliokota jiwe la mali na hatimaye alifariki baada ya kupata presha.

Baada ya kifo, Zunde, Masantula, Da Zu una Pili aliamua kuhama nyumba na walihamia kwenye nyumba mpya. Wakati walivyokuwa wanalipa kodi waligundua kwamba nyumba hiyo ni ya Msauzi na pia kwamba Msauzi ni kaka yake na Zunde na Da Zuu.

Hilo jambo liliwashangaza wote, na Zunde zaidi kwasababu aligundua kwamba mke wake, Pili, alishatembea nay eye na pia na kaka yake. Kwa jinsi ya kuomba msamaha, msauzi aliamua kumpa Zunde nyumba pia na milioni 40, ilimsamehe. Baada ya kupokea hizo pesa, Zunde na Masantula walipiga starehe mpaka pesa zikaisha kwa siku moja. Sasa Msauzi aliamua kumkabidhi Pili pes ana Pili anawasiwasi kwamba Zunde ajamsamehe. Je itakuwaje?

Burudika na vichekesho vya #MMBKitimtim kila Jumatatu na Ijumaa saa 3:30 usiku.