Logo

“The Red Book” – Karma

Habari
23 Machi 2021
Lorenzo aja kwa Desire kudai kwamba ameona “red book” ambayo ina siri zote kuhusu wazazi wake.
debby hudson i1zeyLkx4S0 unsplash

Tangu mwanzo wa #KarmaTZ tumeona kwamba Desire amekuwa akijaribu kujua ni nini kilichowatokea wazazi wake mpaka kufariki. Mama yake mdogo na mjomba wake wamejaribu kumficha na hap ana pale amejaribu kupata majibu bila mafanikio.

 

Lakini wiki iliyopita Lorenzo alikuja kwa Desire kumbwambia kwamba alipokuwa kwa baba yake, Mr. Sendi, aliona kitabu kilichoandikwa “Red Book” au kwa Kiswahili kitabu chekundu. Ndani ya hicho kitabu kulikuwa na siri nyingi ambazo zilifununiwa. Kitabu kiliongelea jinsi Mr. Sendi na Veronica walivyokuwa wahusika wakuu kwenye kifo cha wazazi wa Desire and kwamba wao wawili ndio waliochukua mali za wazazi wa Desire na kumuacha Desire awe yatima na masikini.

 

Lorenzo alivyomwambia haya yote Desire, alikasirika kwasababu Lorenzo anatabia ya uongo. Kwasababu hiyo Desire hakumuamini na alifikiri ilikuwa mbinu nyingine yak wake yeye kumpata Desire tena. Sasa Lorenzo ameapa kutafuta hiki kitabu na kumletea Desire, lakini hiki kitabu kimefichwa na Mzee Sendi na Mzee sendi ameshamfukuza Lorenzo nyumbani kwake.

 

Unafikiri Lorenzo ataweza kupata hiki kitabu na kumuonyesha Desire ukweli? Usikose kuangalia #KarmaTZ kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo. Na pia unaweza kuangalia vipindi vyote vya Karma kwa njia ya Showmax.