Logo

Moto umewashwa na Karma Ndani ya #MMBongo

Habari
05 Agosti 2020
Kipindi cha kwanza na cha pili cha Karma cha aanzisha moto mkali sana hapa Maisha Magic Bongo.
Karma Promo Image

Jumamosi iliopita tuliona mwanzo wa kipindi cha kwanza cha Karma. Karma ni kipindi ambacho kimekuwa kina subiriwa kwa hamu sana hapa nchini Tanzania. Mwezi wa saba kumeona jinsi mitandao yote ilivyokuwa ikivutia kipindi hiki, na kwa kweli watazamaji hawakuvunjwa mioyo kabisa na kipindi.
Karma ilianza na utambulisho wa madaktari bingwa toka India waliosema utaalamu huko ili kurudi nchini na ongeza ujuzi. Moja kwa moja Dr Desire Dustan aonekana kama nyota kwa jinsi  alivyo kuwa juu kwenye masomo yake na urembo wake. Maisha ya Dr Desire kwa mtu wa nje yanaoneka kama yamekamilika lakini na yeye pia ana siri zake. La kwanza, kila mtu anashaanga ni vipi ameweza kufika mbali ki kazi bila kuwa na familia, marafiki au mume wa kumsahidia. Kwenye hii kipindi cha kwanza tunapata upenyo kidogo kwa jinsi mapenzi yanavyo muumiza Dr Desire tukiona uhusiano wake kidogo na  Lorenzo ambae sie muaminifu. Pia Dr Desire akutana na mtoto wa waziri Derick, lakini Derick pia sio muwazi kwa jinsi anavyo mtongoza Dr. Desire.
Balaa la moto mkali umeanza hapa Maisha Magic Bongo na watazamji wetu wana haya kusema kuhusu kipindi cha kwanza cha #KarmaTZ
Usikose kuangalia Karma kila Jumamosi na Jumapili saa 3:00 na marudio kila Alhamisi na Ijumaa saa 2:00 usiku hapa DStv chaneli 160