Logo

Misa anataka kulipiza kisasi – Karma

Habari
30 Machi 2021
Baada ya kugunduliwa kwamba anaongopa kila mtu amkasirikia Misa
Screenshot 2021 03 30 at 21

Kwa muda mrefu Misa alikuwa akidanganya kwamba ana mimba ya mapacha ya Derrick na yupo tayari kuolewa nae. Derrick alimkataa Misa kabisa kwasababu anataka kuwa na Desire lakini Madam Veronica, mama yake na Derrick alimlazimisha Derrick kumuoa Misa. Dada yake na Derrick, Nama alijichukulia jukumu la kumuumbua Misa baada ya kujifunza kwamba Misa hakuwa mjamzito. Lakini ukweli ulitoka na Misa aligundulika kuwa na mimba ya mwezi mmoja na sio miezi mitano. Hicho kitendo kimfanya familia nzima ya Derrick kumutimua Misa na Misa kukarika zaidi na kuapa kulipiza kisasi.

 

Madam Veronica

Misa amekasirika nae kwa sababu baada ya kugundua kwamba Misa alidanganya kuhusu mimba yake, Madam Veronica alimtimua kwake na Misa aliapa kurudi.

 

Nama

Nama ndiye aliye mwambia madam Verocina Pamoja na familia nzima kama Misa hakuwa mjamzito.

 

Khizzer

Tatizo kubwa kwa Khizzer ni kwamba alikataa kudanganya familia yake kwa kutoa vipimo vibovu ili Misa asiumbuke.

 

Shami

Shami alirudiana na Derrick na Misa ana hisi kama hatoweza kumpata Derrick tena.

Unajua kwamba unaweza kuangalia #MMBKarma kwa njia ya Showmax muda wowote, sehemu yoyote.