Logo

Derrick Hataki Kuoa – Karma

Habari
12 Novemba 2020
Misa amevunjika moyo baada ya Derrick kuachana nae baada ya Derrick kukutana na Dr Desire!
Derrick_Karma

Misa na Derrick walikuwa wanaonekana kwamba ni wapenzi wenye msimamo wao na hamna chochote ambacho kingeweza kuja kati kati yao. Lakini Derrick alivyo kataa kuendelea na mipango ya kumuoa Misa ndio kweli matatizo zaidi ndani ya mahusiano yao yalianza kuwekwa wazi.

Misa na Derrick walianza mapenzi yao pale Misa alivyo mnyanganya Derrick toka kwa rafiki yake, shami. Na kama msemo unavyoenda, “jinsi unavyompata mwanaume ndio jinsi utakavyomkosa mwanaume”. Hii inaoneka kwamba ni kweli kwa jinsi Derrick alivyo anza kukosa hamu na Misa baada ya kudata kwa Dr Desire.                                                                                                                                                                                                                     

Ingawa Dr Desire hataki mahusiano na Derrick, Derrick bado anamsumbua. Ameweka wazi kwa marafiki zake kwamba ameona chombo kipya kwa Dr Desire na jinsi akipanda cheo anahitaji mwanamke anaye jitambua kama Dr Desire. Hili jambo limemkarisha sana mama yake, ambaye alikuwa anataka Derrick amuoe Misa. Ingawa Derrick ameweka msimamo wake, unafikiri mama yake ataweza kumlazimisha amuoe Misa?

Usikose kuangalia #KarmaTZ kila Jumamosi na Jumapili saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic

Bongo chaneli 160 na marudio kila Jumatano na Alhamisi saa 2 usiku.