Logo
kapuni
channel logo dark

Kapuni

160DramaPG13

Watazamaji wa #MMBHuba waamua kama Carlos na Sidi wawe pamoja

Habari
29 Aprili 2021
Carlos anampenda Sidi lakini umri wao ndio tatizo kubwa.
Screenshot 2021 05 04 at 11

Baada ya Kashaulo kumuacha Sidi, hili jambo lilimuumiza Sidi sana. Na kipindi hiki, mahusiano kati ya Carlos na Annette. Hatimaye jambo hili lilifanya Carlos na Sidi kuwa karibu.

Kwasababu Sidi na Carlo walikuwa majirani, mahusiano yao yalizidi na ukaribu kati yao ulizidi. Hatimaye Carlos alianza kumpenda Sidi lakini Sidi alikuwa na wasiwasi na umri wake. Carlos ni kijana wakati Sidi ameshakuwa mama. Ingawa wanapenda wanahofu kubwa kwenye mahusiano yao. Tuliawaomba watazamaji wa #MMBHuba kutoa maoni yao kama wanafikiria Carlos na Sidi wawe Pamoja:

  1. “Kwenye umri kuna shida lakini ndo anafanya mambo yawe magumu” - @zainabhamza884
  2. “Sidi hahemi mbele ya Bw. Kashaulo” - @nnabahati
  3. “Carlos hana swag nzuri” - @shagy_bombastic
  4. “Sidi anampenda sana mzee Kashaulo” -@6381_christina
  5. “Ampe tuu mbona Tesa anapenda vijana” -@emmyhg1234
  6. “Ampe tuu kwani ni shingapi?” -@damyt_15
  7. “Hapana,ampotezee manake Kashaulo kashapata begi la hela kwa Kibibi” -@teresafredi7
  8. “Carlos nae atafute size yake, anapenda wamama tuu” -@evesassy80
  9. “Hajielewi huyo Sidi” -@laty_nyembo
  10. “Mapenzi hayachagui umri, ila penzi lao haliendi popote” -@christopherngabine

 

Usikose kufuatilia #MMBHuba kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku ndani ya Maisha Magic Bongo.