Logo
Kapuni slim
channel logo dark

Kapuni

160DramaPG13

Msanii Alice Kibopile -Kapuni

Habari
25 Novemba 2019
Alice anaongea kuhusu mwanzo wake katika tamthilia ya Kapuni, wasanii anaowapenda katika tamthilia hio na nyimbo alizotunga.
Screenshot 2019-11-27 at 11.38.39

Kwenye tamthilia ya Kapuni yeye hutumia  jina la Alice. Alipoanza kuhusika kwenye kipindi cha Kapuni , hakuwa na ujuzi wa kuigiza. Asema kuwa alipopata nafasi ya kuigiza kwenye kipindi,  alipatwa na hofu kwa vile hakuwa na ujuzi wa kuigiza. Asema kuwa hakujua kuwa ana kipaji cha kuigiza .Lakini Director wa kipindi alipo mpa nafasi alifurahia na kwa  hivi sasa anachukua hiyo nafasi anayo kwa umuhimu .Maishani mwake hakuwa anafikiria siku moja atakuwa muigizaji. 

Kunazo changamoto zozote? Alice asema kuwa hii kazi inabidi mtu awe wa Subira kwa vile wasanii wenzake wakati mwingine huwa wanachelewa na inabidi wasubiri lakini kwa yote anadhamini fulsa ambayo anayo. 

Asema pia kuwa kufanya kazi na wasanii wakubwa kama Jordan inamfurahisha sana na kumtia moyo .Kuhusu nyimbo zake , asema anapenda kuimba. Amerekodi nyimbo kadhaa kama ile huchezwa katika tamthiia ya Kapuni, “ Maisha ni Safari ndefu.” 

Usikubali kupitwa kila Jumamosi na Jumapili saa 3 Usiku na marudio yake kila juma pili kuanzia saa 7 mchana